Ticker

6/recent/ticker-posts

JAMII ZISHIRIKIANE NA WATAALAM KWA USTAWI WA MAENDELEO BORA


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

KATIKA kuhakikisha jamii inaendelea kuimarika na kuwa na afya bora pamoja na kuendelea kiuchumi katika nyanja mbalimbali haina budi kushirikiana kwa ukaribu zaidi na wataalamu mbalimbali nchini.

Dkt. Doto Kuhenga ambaye ni Mkuu wa Mawasiliano na Masoko, Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) amefafanua hilo katika Siku ya Ufunguzi wa Maadhimisho ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika Kitaifa jijini Tanga ambayo yameshirikisha Taasisi za Elimu zaidi ya 300 nchini.

Dkt. Kuhenga amebainisha kwamba wataalamu mbalimbali wanaozalishwa kutoka chuo hicho wamekuwa wakifanya mengi ya kuendeleza jamii katika nyanja muhimu katika maisha ya kila siku ndani ya jamii.

"Hii ni Taasisi bora kabisa ya elimu ni bobevu ambayo bado inaendelea kutoka elimu na imeshazalisha wataalamu wengi na tumekuwa tukitoka huduma sana kwa jamii, kwahiyo chuo kikuu hakipo kama kisiwa bali ni kwa ajili ya wananchi" amesema.

Aidha amefafanua kwamba maonesho hayo ambayo yameratibiwa na Wizara ya Elimu kwa lengo la kutoka na kuendeleza vyuo vya elimu ya juu, ubunifu na na vyuo vya kati lakini pia kuonesha ujuzi na ubunifu mbalimbali unaofanywa kupitia sekta ya elimu.

Hata hivyo Dkt Kuhenga amesema maonesho haya yanaleta manufaa Kwa wadau kuweza kufahamu programu pamoja na tafiti mbalimbali zinazoandaliwa na kufanywa kupitia vyuo mbalimbali nchini.

Naye Julio Nyakunga, mwanafunzi aliyehitimu chuo hicho amefafanua kwamba wamekuja katika maadhimisho hayo kuwasilisha mfumo wao mpya ambayo unaangalia visababidhi vya sumu kuvu kwenye madhara ya chakula.

"Hii ni sumukuvu ni sumu ambayo inasababishwa na fangasi ambayo ina madhara kiafya, ambapo inaleta tatizo la ini lakini pia ugonjwa wa ufumavu kwa watoto wadogo,


"Lakini tukija kwa upande wa kiuchumi, sumu hii husababisa kushuka kwa thamani ya mazao yetu ya nafaka uasa Kwa nje ya nchi, yanapopelekwa kuuzwa nje ya nchi, ikipimwa sumukuvu inakuwa kiasi kikubwa hivyo kumwagwa au kuchokwa moto" amesema.


Hivyo amebainisha kwamba kupitia mfumo wao huo ambayo unaonesha visababidhi kwenye madhara ya chakula wanaweza wakakuza uchumi wa Taifa lakini pia kuimarisha afya za wananchi.

Post a Comment

0 Comments