Ticker

6/recent/ticker-posts

SUZA, CHUO KILICHO AZIMIA KUONGEZA PRIGRAMU, ELIMU, UJUZI NA UBUNIFU.


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

MAKAMO Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Taifa Zanzibar (SUZA) amesema chuo hicho kimeazimia kuongea programu mbalimbali kwenye maonesho ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika Kitaifa jijini Tanga kwa lengo la kutekeleza sera na mipango iliyopo kwa Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maadhimisho hayo, Prof. Mohamed Makame haji amesema programu hizo zinakwenda kuangalia hasa kwenye tafiti ambazo zimejiwekeza zaidi kwenye eneo la utekelezaji wa shughuli zinazoendanda na sera ya uchumi wa buluu kama uvuvi, masuala ya gesi asilia pamoja na petroli na mengineyo.


Pamoja mambo mengine Prof Makame amesema vijana wa chuo hicho wana kazi ya kubuni na kuja na suluhisho la aina mbalimbali la kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii, majawabu yanayoweza kutumika kwa jamii na kutoka matokeo zaidi ya kunufaisha Taifa


"Chuo hicho kitaonesha mambo mbalimbali yanayofanywa na Taasisi hiyo ambapo sehemu ya masuala hayo ni kukaribisha utafiti na ubunifu, watu mbalimbali pamoja na wadau wa elimu kufika kwenye chuo hiki kuja kupata huduma ambazo zinatolewa,


"Moto wa chuo hicho ni kichochea katika mabadiliko ya kijamii na oimejikita hapo kuhakikisha kwamba elimu ya juu unaweza kutumika kikamilifu" amesisitiza Prof Makame.

Post a Comment

0 Comments