Ticker

6/recent/ticker-posts

SHIRIKA LA THPS LAWAPIGA JEKI WADAU WA MAT, WAKUTANA KUJADILI URAIBU


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

SABABU ya kuongezeka kwa waraibu wa dawa za kulevya katika Mkoa wa Tanga imetajwa kuwa ni kutokana na Mkoa huo kuwepo mpakani hivyo kuwa na njia za panya kupenyeza dawa hizo.

Lakini pia wasafirishaji ambayo wanatumika kuwa kulipwa dawa hizo kama ujira wa kusafirishia jambo ambalo linaongeza watumiaji katika maeneo hayo kwani hawana mahala pakwenda kuuzia.

Kaimu Kamishna wa Kinga na Tiba, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Dkt. Casian Nyandindi amwyasema hayo kwenye mkutano wa wadau wa huduma za waraibu (MAT), Mkoa wa Tanga uliofanyika jijini humo.

"Tulijua Mkoa wa Dar es salaam unaongoza kwakuwa una watu wengi, lakini Tanga unaongoza Kwa matumizi ya dawa za kulevya, tunapaswa kuwapa elimu ya kutosha juu ya madhara ya dawa hizi,

"Dawa hizi zinachangia Kwa kiasi kikubwa kuleta tatizo la afya ya akili, lakini pia wapo wenye tatizo hili ambayo wanakwenda kutumia dawa za kulevya, tusikate tamaa kuwaelimisha wale ambayo bado hawajazidiwa ukimsaidia mraibu umesaidia jamii nzima" amesema.

Hata hivyo Dkt. Nyandindi amebainisha kwamba matumizi ya dawa za kulevya ni mtambuka hivyo kila mmoja anapaswa kuwajibika kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria katika kutimiza wajibu wake.

Naye Dkt. wa magonjwa ya akili, ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Dawa za Methadone, Dkt. Warles Karata amesema Mkoa umepata athari kubwa kutokana na ongezeko la matumizi ya dawa hizo.

"Serikali imeona waraibu waliopo waweze na kupatiwa dawa, na wale ambayo wameitika na kuanza dawa wanaendelea vizuri na maisha wakiwa na familia zao,

"Tuna Asas za kiraia ambazo zinapambana na waraibu katika mitaa yao, lakini bado tunahitaji Taasisi mbalimbali ziweze kuliona hili na kuweza kuwa msaada kwa hawa waraibu" amesema.

Meneja wa Wadau wa huduma za Waraibu (MAT) Mkoa wa Tanga, Dkt. Otmar Massawa amesema wamejipanga kuhakikisha wanaongeza jitihada katika kushuhulikia kwa ufanisi matumizi mabaya ya dawa za kulevya.

Dkt. Otmar Massawa amewasilisha taarifa ya maendeleo ya mpango huo tangu kuanzishwa kwake na kusema wapokea huduma 1,113 walijiandikisha na 683 wanaendelea na huduma.

Amebainisha kwamba kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kubadilisha maisha ya watumiaji wa dawa za kulevya lakini kuna tatizo la ukosefu wa vituo vya kutolea huduma hizo.

"Hata hivyo nina imani kwamba, mkutano huu utatoa furaha kwa wadau wa (MAT) mikoani hapa na kujadili matatizo yaliyopo ikiwa ni pamoja na kumtafuta suluhu ili kupunguza madhara katika jamii ambayo yanawakabili waraibu wa dawa za kulevya" amesema.

Kwa upande wa waraibu wanaopokea huduma wametoa ushuhuda kuhusu maisha yao ya uraibu na jinsi MAT ilivyowasaidia kurudi katika maisha yao ya kawaida.

Mkutano huo umewezeshwa na Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) chini ya mradi wa Afya Hatua unaofadhiliwa na Mpango wa Dharura wa Rais wa nchi ya Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR), kupitia Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (U.S. CDC).

Post a Comment

0 Comments