Ticker

6/recent/ticker-posts

ULINZI NA USALAMA WA PESA ZENU UPO MIKONONI MWENU

Wafanyabiasha wa Kijiji na Kata ya Halungu wilayani Mbozi mkoani Songwe wametakiwa kuwa makini dhidi ya matapeli wa wizi kwa njia ya mitandao ili kuepuka kupoteza mali zao.

Akizungumza wakati akitoa elimu ya ulinzi na usalama wa biashara zao na umuhimu wa kuchukua taarifa za wateja wanaowahudumia Mei 13, 2024 Polisi Kata ya Halungu Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Micah Mtafya alisema, endapo watafuata na kuzingatia taratibu za huduma za kifedha kwa wateja wao hawatapata madhila ya kuibiwa.

"Ili kutokomeza vitendo vya wizi kwa njia ya mitandaoni mnatakiwa kuwa makini pindi mtoapo huduma ikiwa ni pamoja na kutowakabidhi wateja simu ili waandike namba zao ili kuepuka kubadilisha majina ya matajiri wenu kwa lengo la kutekeleza wizi ambao utawarudisha nyuma katika biashara zenu” alisema Mkaguzi Mtafya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Mariam Nzengula amelishukuru Jeshi la Polisi kwa elimu waliopata na wameahidi kuongeza umakini na kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa pindi waonapo viashiria au wafanyiwapo vitendo hivyo ili kutokomeza uhalifu huo.

Post a Comment

0 Comments