Ticker

6/recent/ticker-posts

WASHINDI WA ZIGO LA EURO CUP NA Hisense DROO YA KWANZA WATANGAZWA

 


 Ramadhan S. Mrutu ( Katikati ) ambaye ni mshindi wa tiketi ( Droo ya kwanza ) Kampeni ya ZIGO la EURO CUP na Hisense, safari iliyolipiwa kila kitu  kwenda kutazama mechi za Kombe la Euro moja kwa moja nchini Ujerumani kuanzia hatua ya 16 bora, akikabidhiwa Mfano wa Tiketi tukio lililofanyika mapema leo hii Mei , 31 , 2024 Makao makuu ya Tigo Jijini Dar Es Salaam , Ramadhan ameibuka mshindi baada ya kubashiri Mechi na PariMatch kupitia Tigo Pesa Super App, Kushoto ni Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Ruta na Kulia ni Erick Gerald kutoka PariMatch.

Na Adery Masta.

Ramadhan S. Mrutu Mkazi wa Dar Es Salaam, ni Mteja wa Tigo wa kwanza kabisa ( Droo ya Kwanza ) kujishindia Safari iliyolipiwa kila kitu ya kwenda kutazama Mechi za Kombe la EURO 2024 , ambapo timu 24 zinatarajiwa kuchuana katika miji 10 mwenyeji Nchini Ujerumani . 

Bahati hii imemfikia Bwn. Ramadhan kutokana na Kampeni ya ZIGO LA EURO CUP NA Hisense , iliyozinduliwa wiki kadhaa Zilizopita ambapo Kampuni ya Mawasiliano ya TIGO, kwa kushirikiana na Parimatch na Hisense waliileta kusambaza Tabasamu kwa Wateja wao.

Ili kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kujishindia tiketi au zawadi ya fedha taslimu TZS 1,000,000, na Vifaa vya Hisense TV na Friji washiriki wanapaswa kujiandikisha na Parimatch, kuweka amana kupitia Tigo Pesa kisha kuweka dau kwenye mechi yoyote ya mpira wa miguu na Parimatch. Kadiri dau zinavyowekwa, ndivyo nafasi zinavyoongezeka ya kushinda TZS 1,000,000 au tiketi ya safari na mechi yenye malipo kamili ya kwenda kutazama mechi za Kombe la Euro moja kwa moja nchini Ujerumani kuanzia hatua ya 16 bora.

Akizungumza Wakati wa Kugawa zawadi kwa Washindi ambao kati Yao ni Washindi wawili wa Kifurushi cha Vifaa vya Kielekitroniki kutoka Hisense ambavyo ni TV janja na Friji la kisasa , Mshindi wa Milioni Moja Pesa Taslimu na Ramadhan ambaye kajishindia Tiketi Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Ruta amesema 

" Ndo kwanza ni droo ya kwanza ya Kampeni yetu ya ZIGO LA EURO na Hisense , kama ambavyo inajulikana Kampeni hii tunafuta Washindi wa Tiketi ya Kwenda kushuhudia Mechi za Euro , Washindi wa Vifaa vya Hisense ambavyo ni Friji na Tv ya Kisasa , na Washindi wa Pesa Taslimu

Zawadi bado zipo nyingi kwa maana Leo ndo Washindi wa Droo ya kwanza, bado Kuna Droo nyingine saba zinawasubiri , Tumia kwa wingi TIGO Pesa Super App , Bashiri na Parimatch kupia App ya Tigo Pesa ili kutengeneza mazingira ya kujishindia zawadi za Tv na Friji kutoka Hisense , Fedha Taslimu Hadi Milioni Moja na Zawadi kubwa ya kwenda kushuhudia Mechi za EURO CUP 2024 " alimalizia Mary RutaKwa upande wao Washindi wa TV na Friji Maureen Shirima , Faustine Mashelle na James Mgonja , Mshindi wa Pesa Taslimu Shilingi Milioni Moja Fredrick Mlayi wameipongeza Kampuni ya TIGO , Parimatch na Hisense kwa ushirikiano unaoleta Furaha kwa Wateja wao , Aidha wamesisitiza kuwa Siri pekee ya Ushindi ni kutumia TIGO PESA super app.

Post a Comment

0 Comments