Ticker

6/recent/ticker-posts

MADABA KUNUFAIKA KIUCHUMI NA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MISITU



Na. John Bera - Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imepongezwa kwa kuendeleza sekta ya Misitu katika Wilaya ya Madaba Mkoani Songea ambapo imepanda zaidi ya hekta laki moja lengo ikiwa ni kuendeleza sekta ya Misitu katika wilaya hiyo.

Hayo yamebainishwa   na  Mbunge wa Mabada, Mhe. Joseph Mhagama wakati akichangia mada kwenye mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Maliasilii inayowasilishwa leo Juni 03, 2024 Jijini Dodoma.

Mhe. Mhagama amesema jitihada hizo zilizofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii zitaleta mapinduzi makubwa kwa wananchi wa eneo hilo ambapo miti iliyopandwa itasaidia kuleta manufaa makubwa  kichumi ikiwemo kuongeza pato la Taifa kwa ujumla.

‘’ Mchango wa uchumi utakaopatikana kwenye  uwekezaji huu kwenye  eneo la Madaba  utaleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa wananchi pamoja na Serikali kwa ujumla ’’ Alisema  Mhagama.

Aidha ameongeza kuwa, kwa kutambua jitihada zilizofanywa na wizara, Halmashauri ya Wilaya ya Madaba imechukua hatua kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ambapo imeandaa mpango maalumu wa kujenga kongani la viwanda vya bidhaa za mbao ambapo  hekari 25 zimeshatengwa kwa ajili ya kujenga kongani hilo.

Ameongeza kuwa uwekezaji katika  Kongani hilo katika Wilaya ya  Madaba unamanufaa kwenye mnyororo mzima wa thamani wa  mazao ya misitu ambapo zaidi ya watu laki moja na elfu Hamsini watakuwa na uwezo wa kupata ajira.

‘’Matokeo yatakayotokana wa Kongani  ni kutoa ajira kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu ambapo tunarajajia zaidi ya watu laki moja na nusu watapata ajira ambapo ni zaidi ya idadi ya watu waliopo katika Wilaya ya Madaba’ Alisema Mhagama.

Sambamba na hayo, Mhe. Mhagama ameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii kusaidia kutangaza uwekezaji katika eneo hilo ili waweze kupata watu walio sahihi wa kuwekeza katika eneo hilo litakalokuwa na manufaa ya wakazi wa eneo hilo.

Uwekezaji wa upandaji miti Madaba, ni wapili  kwa ukubwa mara baada ya Uwekezaji uliowekwa katika Shamba la Sao Hill ambapo Serikali iwekeza katika eneo hilo.

Post a Comment

0 Comments