Ticker

6/recent/ticker-posts

SHERIA MPYA YA UWEKEZAJI ILIVYOWAVUTA WAWEKEZAJI WAZAWA.


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

SHERIA mpya ya Uwekezaji ya mwaka 2022, imeleta mwamko mkubwa na kuwavuta wawekezaji wengi wazawa nchini jambo lililoleta ongezeko la uwekezaji wa viwanda.

Kaimu Meneja wa Kituo cha Uwzekezaji (TIC), Kanda ya Kaskazini, Veronica Thadeus amesema mabadiliko ya sheria hiyo yamekuwa chachu kubwa kwa wawekezaji wazawa kujitokeza kuwekeza.


"Tunatekeleza majukumu yetu chini ya sheria yetu mpya ya mwaka 2022 iliyofanyiwa maboresho Kwa lengo la kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji hapa "" amesema.


Kaimu Meneja huyo amefafanya kwamba sheria hiyo mpya imetoa fursa kwa Watanzania, na kwamba hapo awali thamani ya mradi wa Mtanzania ilikuwa ni kiasi cha Dola laki moja ambayo ni sawa na sh milioni 250 ambayo ilikuwa ni garama kubwa.


Kufuatia mabadiliko ya sheria, amesema kwamba kwa sheria mpya thamani ya mradi kwa sasa ni Dola hamsini elfu, ambayo ni sawa na sh milioni 125, hivyo kiwango hicho kimeshushwa na muitikio umekuwa mkubwa.


"Watanzania wameitikia wito na wameweza kusajili miradi Yao na TIC ambapo kwa takwimu zilizopo sasa hivi, asilimia 60 ya wawekezaji ni wazawa ambapo miradi mingine wamechangia na wageni na asilimia 40 ni wageni pekeyake,


"Kwa takwimu hiyo, unaonesha kwamba Watanzania, wamewiwa na wako tayari na wanaendelea kuwekeza katika fursa mbalimbali hapa nchini" amebainisha.


Hata hivyo amesema kwa Mkoa wa Tanga ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, kuanzia mwaka jana hadi mwezi huu wameweza kusajili miradi nane, tofauti na mwaka 2022 ambapo walisajili miradi minne.


Pia amebainisha kwamba miradi iliyotangulia itakapo kwenda kutekelezwa ipadavyo italeta manufaa makubwa kwakuwa inakwenda kuleta ajira zaidi ya 1000 kwa Watanzania.


"Kwahiyo tumeona ni namna gani wakazi wa Tanga ambao wanaizunguuka ile miradi watakwenda kunufaika na ajira, lakini pia miradi hiyo itakapokamilika na kufanya kazi, thamani ya mtaji itakayoenda kuwekezwa siyo chini ya Dola 147 ambazo ni sawa na sh billion 367.5,


"Hivyo tunaona uwekezaji huu ni mkubwa na inakwenda kubadilisha kabisa Mkoa wa Tanga kwa upande wa ajira, tekinolojia lakini pia mlolongo mzima wa uwekezaji mkoani hapa" amesema.


Ameeleza kwamba mabadiliko ya mlolongo huo umechangiwa na uwepo wa mradi wa bandari ya Tanga ambayo pia Wana jukumu la kutangaza.


"Kwa kutangaza kwetu tumeona katika miradi iliyopo wawekezaji wengi wamejikita kuwekeza kwenye kujenga miundombinu ambayo inakwenda kuhudumia huduma zote zinazotolewa na bandari" amesema.

Post a Comment

0 Comments