Ticker

6/recent/ticker-posts

ZAO LA MKONGE LINAHITAJIKA KWA WINGI NCHINI : TSB


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

BODI ya Mkonge nchini (TSB) imeendelea kuwahimiza wakulima kujikita kikamilifu katika kilimo cha zao la Mkonge kwakuwa ni zao ambalo bado linahitajika kwa wingi na lililopo bado ni kidogo.

Lakini pia imeelezwa kwamba zao hilo kwa sasa halina shida kubwa ya soko hivyo kilimo hicho ni fursa kubwa sana kwa kila mwananchi mwenye eneo ambalo anaweza kulima.

Ofisa Biashara wa Bodi ya Mkonge nchini (TSB), David Maghali ameyasema hayo mbele ya mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi, Dkt. Batilda Buriani alipopita kukagua Banda la maonesho la Bodi hiyo katika ufunguzi wa Maonesho ya 11 ya Biashara Mkoa wa Tanga.

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mkonge nchini (TSB), Sady Kambona ametoa ufafanuzi kuhusiana na uvumi wa kuwepo kwa mashamba ya Mkonge kwenye Bodi hiyo.

Kambona amefafanua kwamba kwa muda mrefu sasa Bodi hiyo haina mashamba bali inahimiza na kuwashauri wananchi wenye machamba yao kuendeleza kilimo hicho.

Post a Comment

0 Comments