Ticker

6/recent/ticker-posts

CPA MAKALLA: CCM ITAWALETEA WAGOMBEA WASIO NA MAKANDOKANDO


Na Richard Mwaikenda, Mwanza

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla akiwaahidi wananchi kwamba ikifika wakndiye ati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa mwakani CCM itawapelekea wagombea wenye sifa, wasio na makandokando wenye malengo ya kuwaletea maendeleo.

"Niseme, nisiseme, Niseme nisisemee? Mimi ndiye Katibu Mwenezi wa CCM, nataka niwahakikishie CCM itawaletea wagombea safi, wasio na makandokando ambao wako tayari kuwaletea wananchi maendeleo. Mko tayari, mko tayari?" Makalla aliwahakikishia wananchi hivyo kisha kuwahoji kama watakuwa tayari kuwapigia.

Ametoa ahadi hiyo alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza Agosti 15, 2024 ambao pia ulihutubiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi.

Dk Nchimbi alihitimisha ziara hiyo yenye mafanikio makubwa aliyoifanya katika mikoa minne ya Kigoma, Kagera, Geita na Mwanza.

Tangu ashike wadhifa huo, ameshafanya ziara katika mikoa mingine 13 ambayo ni; Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Lindi na Mtwara.

Katibu Mkuu wa CCM huyo, katika ziara yake hiyo aliyoanzia Mkoa wa Kigoma Agosti 4, 2024, aliambatana na Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Issa Haji Usi Gavu, Katibu wa NEC - Oganaizesheni, Ndugu Amos Gabriel Makalla, Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo na Ndugu Rabia Hamid Abdalla, Katibu wa NEC - Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

Malengo ya ziara hiyo ni; Kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025, kuhuisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua kero za wananchi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki taarifa zao na kujiandikisha katika Kitabu cha Kudumu cha Wapiga kura, kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments