Ticker

6/recent/ticker-posts

TBS YATOA ELIMU KWA UMMA WILAYA ZA MKOA WA ARUSHA.


SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) linaendelea na Kampeni yake Ya kutoa Elimu Kwa Umma katika Ngazi za Wilaya ambapo hadi sasa Shirika hilo limetoa Elimu Kwa wananchi Wafanyabiashara na Wajasiriamali Wadogo Ndani ya Wilaya 93 nchi nzima na Lengo likiwa ni kuzifikia Wilaya Zote nchini.

Akizungumza hivi karibuni katika Wilayani Karatu mkoani Arusha Meneja Wa Uhusiano na Masoko TBS Bi. Gladness Kaseka amesema lengo la Shirika hilo ni kutoa Elimu Kwa Umma katika Ngazi za Wilaya zote.

" Kwa sasa TBS tumeamua kuwafikia Wajasiriamali ,Wafanyabiashara na wananchi katika Ngazi Za Wilaya ili kuwapatia utaratibu unaotakiwa kwa ajili ya kupata alama ya Ubora, kusajili majengo ya Biashara ya chakula na Vipodozi ili kuepuka Usumbufu unaoweza kujitokeza, umuhimu wa kununua bidhaa zenye ubora na namna ya kuwasiliana na TBS wapatapo changamoto yeyote. Elimu hii ya Umma ipo katika ngazi ya Wilaya na hadi sasa TBS imezifikia Wilaya 93, na kwa hapa Arusha tutatoa Elimu katika wilaya za Karatu, Loliondo - Ngorongoro, Longido , Monduli na Arusha yenyewe ". amesema Bi. Kaseka

Aidha Bi. Kaseka amewasihi Wananchi kuhakikisha wanasoma taarifa zinazopatikana katifa vifungashio za bidhaa pamoja na muda wa mwisho wa matumizi na kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS ili kuepuka hasara ya kupoteza pesa na kulinda afya zao.

Hapo awali wakizungumza kwa nyakati tofauti na Vikundi vya Wajasiriamali wanaosindika maziwa na Wanaooka mikate Wilayani Karatu, TBS wameweza kuwapatia utaratibu wa jinsi ya kupata alama ya Ubora ambayo inatolewa Bure, alama itakayowasaidia si tu kukuza Biashara zao , Bali pia kulinda afya za Wateja wao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti Bi. Hoisa Monyo - Katibu wa Kikundi kinachojishughulisha na Usindikaji wa Maziwa na Bi. Matilda Shirima - Katibu wa Kikundi cha Uokaji Mikate, wamelipongeza Shirika la Viwango Tanzania ( TBS ) kwa Elimu waliyoamua kutoa kwa maana imewafumbua Mambo mengi kuhusu umuhimu wa Viwango katika bidhaa wanazozizalisha.

Post a Comment

0 Comments