Ticker

6/recent/ticker-posts

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AONGOZA KIKAO CHA TCD

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, akiongoza Kikao cha Mashauriano cha Vyama vya Siasa Wanachama wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), ambacho, mbali ya viongozi wa vyama hivyo, pia kilihudhuriwa na mawaziri na manaibu waziri wakiwakilisha upande wa Serikali.

Baadhi ya viongozi wakuu wa vyama hivyo walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Chadema, ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCD kwa sasa, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Ndugu Dorothy Semu, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Ndugu Joseph Selasini, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR - Mageuzi.

Upande wa Serikali, uliwakilishwa na Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Afya, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Festo Ndugange, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Mhe. Daniel Sillo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kikao hicho kimefanyika leo Jumapili, Agosti 18, 2024, jijini Dar Es Salaam.

Post a Comment

0 Comments