Ticker

6/recent/ticker-posts

MATUMIZI YA MKAA, KUNI DAR ES SALAAM TISHIO KWA MISITU KISARAWE, TaTEDO-SESO WATOA ELIMU YA UVUNAJI ENDELEVU

Na Mwandishi Wetu 

Afisa Misitu msaidizi wa Wilaya ya Kisarawe Bwana Waziri Mkumbwa amesema hali ya uvunaji wa misitu kwa ajili ya nishati ya mkaa na kuni imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na hitaji kubwa ya nishati hiyo katika mkoa wa Dar es Salaam. 

Amesema kwa mwaka huu (2024) Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe imekusudia kupunguza uvunaji. 

 Taasisi isiyokuwa ya kiserikali inayojishugulisha na Uendelezaji wa Teknolojia na huduma ya nishati Endelevu (TaTEDO-SESO) imewafakia wavunaji wa mkaa wilayani Kisarawe na kuwapa Elimu ya uvunaji endelevu katika mnyororo wa thamani ya mkaa bila kuathiri misitu. 


Akizungumza baada ya kutembelea maeneo ya uchomaji wa mkaa katika kijiji cha Sofu Wilayani humo, Mratibu wa Miradi wa TEDO-SESO Bwana Shima Sago amesema wamelenga kuwafundisha wachomaa mkaa jinsi ya kuvuna kiendelevu bila kuathiri misitu ikijumyisha namna ya kuchagua aina ya miti ya kuvuna na kutovuna miti yenye thamani, kuacha maotea ya miti, kuacha miti yenye makazi ya ndege na wanyama.


Mbali na Elimu ya uvunaji wa endelevu wa misitu pia TaTEDO-SESO imetoa Elimu ya matanuru bora ya kienyeji yenye mfumo wa kutoa moshi kupitia bomba kwa ajili ya kulinda Afya ya mchomaji mkaa kutoka kwenye hatari ya kupata maradhi ya Kifua Kikuu (TB) unasababishwa na hewa chafu inayotokana na matanuru ya mkaa. Pia Bwana Shima amesema matanuru hayo yanelenga kuwasaidia wachomaji mkaa kuvuna mkaa mwingi na uliobora. 

Jitihada hizo zinalenga kuhakikisha uvunaji wa misitu kwa ajili ya nishati unazingatia uhifadhi endelevu katika wakati wa mpito wa kuhamia matumizi ya nishati safi wa gesi na umeme kama ilivyo agenda ya Serikali. 

 Uvunaji wa misitu kwa ajili ya mkaa kutoka magunia 350,000 yaliyovunwa kihalali mwaka jana (2023) hadi kufikia magunia 220,000. Hata hivyo ameongeza kuwa idadi hiyo itazidi kupungua mwaka hadi mwaka kufuati Elimu ya uhifadhi wa mazingira na matumizi ya nishati mbadala inayoendelea kutolewa na serikali wilayani humo kwa kushirikiana na wadau. 


Aidha ameongeza kuwa katika jitihada za uhifafhi wa mazingira na kurejesha uoto ulioharibiwa, Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe imelenga kupanda miti Milioni moja na laki tano kila mwaka.

Post a Comment

0 Comments