Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi wa Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo, akitoa elimu ya fedha kwa wananchi kuhusu umuhimu wa usimamizi wa fedha binafsi, jinsi ya kupanga mapato na matumizi ili kuweka akiba na kujikwamua kiuchumi pamoja na kujiandaa na maisha ya baadaye, wakati Maafisa wa Wizara ya Fedha walipokuwa wakitoa elimu ya fedha kwa wananchi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Chalinze.
******************
Afisa Maendeleo ya Jamii na Msajili Msaidizi Vikundi vya Huduma Ndogo za Fedha, Halmashauri ya Chalinze, Bi. Flora Barakana, akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliohudhuria katika programu ya utoaji elimu ya fedha kwa wananchi inayotekelezwa na Wizara ya Fedha, kuhusu namna ya kusajili vikundi na kuwawezesha kupata fursa ya mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Serikali, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Chalinze
0 Comments