WAZIRI MKUU na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Kassim Majaliwa amewahimiza Wana-Liwale na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 nchi nzima na kuwachagua wagombea wote wa Chama cha Mapinduzi.
Amesema hayo leo (Jumanne, Novemba 26, 2024) wakati alipofunga kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa zilizofanyika katika viwanja vya ujenzi, Liwale Mkoani Lindi.
Amesema kwa kufanya hivyo ni kutimiza haki ya msingi katika kuwachagua viongozi watakaowatumikia katika kipindi cha miaka mitano “Huu ni wakati muhimu wa kufanya uchaguzi wa viongozi bora ambao wataleta maendeleo ya kweli, nendeni mkachague viongozi waliowekwa na CCM”
Amesema kuwa CCM inaamini kwa kuwachagua viongozi wa chama hicho itawawezesha kuwa na viongozi wa kipekee, wanaojali na wanaohakikisha kuwa uwajibikaji na maendeleo vinapatikana kwa kila mwananchi.
“Hivyo basi, tutumie haki yetu ya kidemokrasia kwa kuchagua viongozi bora na kwa umoja kuhakikisha kuwa tunaendelea mbele kama taifa”
0 Comments