Ticker

6/recent/ticker-posts

FAMILY DAY 2025 YA MGODI WA BARRICK BULYANHULU YAKUTANISHA FAMILIA ZA WAFANYAKAZI NA JAMII KUFURAHI PAMOJA

 
Kaimu Meneja Mgodi wa Barrick Bulyanhulu  Leon Ebondo akizungumza wakati Barrick Bulyanhulu Family Day
**
Mgodi wa dhahabu wa Barrick Bulyanhulu uliopo katika halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga umeandaa tukio la Family Day 2025, ambalo limekutanisha mamia ya wanafamilia wa wafanyakazi wa Mgodi huo ,viongozi wa Serikali na vijiji vinavyozunguka mgodi  na wakazi wa eneo hilo ambapo wameungana na kufurahi pamoja.

Tukio hilo ambalo hufanyika kila mwaka mwishoni mwa mwezi Desemba lilipambwa na maonesho ya shughuli zinazofanyika katika mgodi huo, michezo mbalimbali ya watu wazima na watoto, chakula cha pamoja, vinywaji , muziki na kubadilishana mawazo.

Kaimu Meneja Mgodi wa Barrick Bulyanhulu  Leon Ebondo ,amewakakaribisha na kuwashukuru wote waliohudhuria hafla hiyo ambayo imewezesha wanafamilia za wafanyakazi kuona kazi zinazofanywa na mgodi sambamba na kudumisha mshikamano na jamii inayozunguka mgodi huo.
 
Nao baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo wamepongeza mgodi huo kwa kuandaa siku hiyo kubwa ambayo mbali na kujumuisha wafanyakazi na familia zao pia inawaunganisha na viongozi wa vijiji jirani na wananchi wanaoishi katika eneo hilo.

Post a Comment

0 Comments