Ticker

6/recent/ticker-posts

FEITOTO AIPELEKA STARS HATUA YA MTOANO AFCON


Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars imefanikiwa kufuzu hatua ya mtoano ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) kwa mara ya kwanza kwenye historia tangu michuano hiyo ianzishwe mwaka 1957 baada ya kulazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Tunisia.

Bao pekee la Taifa Stars limefungwa na nyota Feisal Salum "Feitoto" dakika ya 48 ya mchezo.

Taifa Stars imefuzu hatua hiyo kwa njia ya "Best Loser" baada ya kumzidi Angola kwenye kigezo cha idadi ya mabao ya kufunga

Mchezo unaofuata katika hatua ya 16 bora Stars watakipiga dhidi ya Wenyeji wa michuano hii Timu ya Taifa ya Morocco.

Post a Comment

0 Comments