
Na Mwandishi Wetu
VIONGOZI wa Dini wana nafasi kubwa ya kuunganisha jamii kutokana na madhara yaliyotokea katika Uchaguzi Mkuu na baada ya uchaguzi.
Hayo ameyasema Mwalimu na Muumini Kanisa Katoliki Ludoovick Joseph wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema katika hatua iliyokuwepo viongozi wa dini kuendelea kuwajenga kiimani waumini katika kuhakikisha amani inakuwepo wakati wote.
Amesema kuwa wakati Serikali inakwenda katika maridhiano mchango wa viongozi wa dini ni muhimu kwani wao ndio wananchi wengi wanaongoza kwenye imani ya kiroho.
Joseph amesema nafasi walionazo viongozi wa dini kama kuna changamoto wanaweza kuzitumia na sio kuwagawa wa waumini.
Mwalimu Ludovick Joseph, amesema viongozi wa dini wana haki na wajibu wa kiroho kukemea maovu yanapotokea katika jamii ili kujenga dhamiri za waumini na kutoa mwelekeo wa kimaadili kwa Taifa.
"Kasoro kubwa inayojitokeza ni matumizi ya lugha, uongeaji wa viongozi wa dini haupaswi kufanana na lugha ya wanasiasa au wapinzani wa kisiasa, bali uwe wa kidini, kichungaji na wa kimaadili," amesema.
Amefafanua kuwa viongozi wa dini wanapaswa kutumia lugha ya upendo, maridhiano na hekima, huku wakiepuka kauli zinazoweza kuchochea migawanyiko au kuleta taharuki katika jamii.
0 Comments