Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YATOA SIKU 90 WAMILIKI KUSAJILI MAENEO YA KAZI OSHA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, akizungumza na watumishi wa OSHA kwenye ziara ya kikazi katika Ofisi za OSHA Dar es Salaam.

***************

Na Mwandishi Wetu

Serikali imewataka wamiliki wa maeneo ya kazi nchini ambao maeneo yaohayajasajiliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kusajili maeneohayo ndani siku tisini kuanzia Januari 2026.

Agizo hilo la serikali limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira naMahusiano, Deus Sangu alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za OSHA zilizopoKinondoni Jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo ambayo ni ya kwanza kwa Taasisi ya OSHA tangu Waziri huyo alipoteuliwana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kusimamia masuala ya kazi nchini, imelengakujifunza jinsi OSHA pamoja na Taasisi nyingine chini ya Wizara yake zinavyotekelezamajukumu yake.

Akizungumza na menejimenti na watumishi wa OSHA leo (Desemba 22, 2025), WaziriSangu amesema Taasisi ya OSHA inayo dhamana kubwa ya kulinda nguvukazi ya Taifa dhidi ya ajali, magonjwa na vifo vitokanavyo na mazingira ya kazi yasiyokuwa rafiki.

Aidha, Waziri Sangu amesema ili OSHA iweze kusimamia ipasavyo uzingatiaji wakanuni bora za usalama na afya katika maeneo ya kazi nchini maeneo hayo yanapaswakutambulika na OSHA kupitia usajili.

Aidha, Waziri huyo amewataka watumishi wa OSHA kufanya kazi kwa bidii, kujituma nakuzingatia weledi katika kuwawezesha waajiri kusimika mifumo madhubuti ya usalamana afya mahali pa kazi huku akiwataka waajiri hao kuzingatia ushauri ambao umekuwaukitolewa na wataalam wa OSHA.

“Usajili wa sehemu za kazi nchini ni kwa mujibu wa kifungu cha 16 na 17 cha Sheria yaUsalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 ambapo OSHA husajili maeneo yakazi na kisha kuyafikia kwa ajili ya ukaguzi na ushauri wa kitaalam juu ya uboreshaji wamazingira ya kazi,” ameeleza Waziri Sangu.

Akitoa maelezo kuhusu Taasisi ya OSHA kwa Waziri, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, amesema yeye na watumishi wa OSHA wamefarijika kumpokeaWaziri na ujumbe wake ambapo watakuwa tayari kupokea maelekezo yote ya serikalina kuyafanyia kazi ipasavyo.

“Kwa niaba ya watumishi wenzangu, nikuhakikishie kwamba hatutakubali kuwa sababuya kukwamisha utendaji wenu bali tutajitahidi kutekeleza majukumu yetu ipasavyo nahivyo kuwafanya nyinyi viongozi wetu kutembea kifua mbele kutokana na utendaji wetumzuri,” ameeleza Kiongozi Mkuu wa Taasisi ya OSHA, Bi. Mwenda.

Waziri Sangu ameambatana na Naibu wake, Rahma Kisuo pamoja na Kamishna waKazi, Bi. Suzan Mkangwa ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

OSHA ni Taasisi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) yenye jukumula kutoa na kusimamia miongozo ya usalama na afya mahali pa kazi ambapo katikakutekeleza jukumu hilo, husajili maeneo ya kazi na kuyafikia kwa ajili ya ukaguzi naushauri wa kitaalam juu ya uboreshaji wa mazingira ya kazi.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo, akizungumza na watumishi wa OSHA kwenye ziara ya kikazi katika Ofisi za OSHA Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa OSHA Bi. Khadija Mwenda, akitoa maelezo kuhusu utekelezajimajukumu ya OSHA wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, katika ofisi za OSHA Dar es Salaam.

Kamishna wa Kazi, Bi. Suzan Mkangwa ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi yaWaziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Bi. Mary Maganga, katika ziara ya Waziri waWizara hiyo, Mhe. Deus Sangu katika Ofisi za OSHA Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu naNaibu wake, Mhe. Rahma Kisuo, baada ya kupokelewa na watumishi OSHA katika Ofisi za Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, Naibu wake Mhe. Rahma Kisuo wakishiriki sala ya ufunguzi wa kikao chao nawatumishi wa OSHA wakati wa ziara ya kikazi katika Ofisi za OSHA Dar es Salaam. Viongozi wengine katika meza kuu ni Kamishna wa Kazi, Bi. Suzan Mkangwa, MtendajiMkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara OSHA, Bw. Raphael Makoninde.

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda akiwa pamoja na Mkurugenzi waHuduma za Biashara OSHA, Bw. Raphael Makoninde.

Watumishi wa OSHA wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, wakati wa ziara ya kikazi katika Ofisi za OSHA Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi yaWaziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, vifaa kinga (Personal Protective Equipment-PPEs) ambavyo atakuwa anavitumia anapotembelea maeneo yakazi kwa ajili ya ukaguzi wa mifumo ya usalama na afya.

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akimkabidhi Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo, vifaa kinga (Personal Protective Equipment-PPEs) ambavyo atakuwa anavitumia anapotembelea maeneo yakazi kwa ajili ya ukaguzi wa mifumo ya usalama na afya.
 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, akisalimiana na watumishi wa OSHA mara baada ya kuwasili katika Ofisi za OSHA Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi.

Post a Comment

0 Comments