Ticker

6/recent/ticker-posts

Bandari ya Pemba kufungua zaidi milango ya utalii

Na Mwandishi Wetu

PEMBA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema Pemba ina vivutio vingi vya utalii hivyo ujenzi wa Bandari yaMkoani, Pemba itafungua zaidi milango katika sekta mbalimbali.

Mhe. Masauni amesema, Bandari ya Mkoani ni kiunganishi na muhimili wa maisha ya kila siku ya wananchi wa Pemba, ni lango la biashara, elimu, afya, utalii na mshikamano wa kijamii katiya Pemba, Unguja na Tanzania Bara.

Ameyasema hayo Januari 10, 2026 wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo jipya la kisasa la abiria katika bandari hiyo ambapo jengo hilo litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiriazaidi ya 1,500 na kuinua huduma za bandari kwa viwango vya kimataifa, ikiwa ni shamrasharakuelekea miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 90 ya abiria wanaosafiri kwenda nakutoka Kisiwa cha Pemba hutumia usafiri wa baharini, hali inayoifanya bandari hiyo kuwa naumuhimu kwa ajili ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

“Usafiri wa baharini si mbadala, bali ni mahitaji muhimu ya maisha ya wananchi wetu, ndiyomaana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeona umuhimu wa kuwekeza katika miundombinu yakisasa, salama kwa abiria,” amesema Mhe. Masauni.

Amesema ujenzi wa jengo hilo unatokana na mkataba wa uwekezaji kati ya Shirika la Bandari nawawekezaji wa Fumba Port, akibainisha kuwa ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya Serikali nasekta binafsi katika kuharakisha maendeleo ya miundombinu ya kimkakati.

“Ushirikiano huu unapunguza mzigo kwa Serikali, unaongeza ubora na ufanisi wa huduma, nakuchochea uchumi kupitia ajira kwa vijana na wananchi kwa ujumla,” amesema.

Amewata watoa huduma wa bandari, waendeshaji wa vyombo vya usafiri wa majini pamoja naabiria kuitumia miundombinu hiyo kwa nidhamu, uadilifu na kuitunza ili idumu kwa mudamrefu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo, wakandarasi na wasimamizi wa mradikuhakikisha ujenzi unatekelezwa kwa ubora unaostahili, kwa wakati na kwa kuzingatia thamaniya fedha.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar, Akif Ali Khamis, amesemakukamilika kwa mradi huo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na changamoto yaupatikanaji wa usafiri wa uhakika kwa abiria wanaosafiri kati ya Pemba, Unguja na Tanzania Bara.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, Pemba Mhe. Miza Hassan Faki, amesemauwepo wa bandari hiyo umechangia ongezeko la meli zinazotia nanga katika eneo hilo, akisemakuwa awali bandari ilikuwa inapokea abiria 60,000 kwa mwezi lakini kwa sasa inapokea zaidi yaabiria 100,000.

Ameongeza kuwa bandari hiyo imechangia pia kuongeza ajira kwa wananchi wa maeneo yajirani, hususan vijana ikiwa pamoja na kupunguza changamoto ya upatikanaji wa mafuta ambapoawali uwezo wa kuhifadhi mafuta ulikuwa lita 100,000, lakini kwa sasa umeongezeka hadikufikia lita milioni mbili.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo jipya la kisasa la abiria katika Bandari ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba, Januari 10, 2026.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar, Akif Ali Khamis kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo jipya la kisasa la abiria katika Bandari ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba, Januari 10, 2026.
 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akizungumza na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo jipya la kisasa la abiria katika Bandari ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba, Januari 10, 2026.

PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Post a Comment

0 Comments