Ticker

6/recent/ticker-posts

Vyuo na Viwanda Kushirikiana Kukuza Ujuzi na Ajira kwa Vijana

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ametoa wito kwa sekta binafsi kushirikiana na Vyuo,kuwekeza katika tafiti hususan za sayansi na teknolojia ili kuinua viwango vya tafiti na ubora wa elimu nchini.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa uzinduzi wa mpango wa ushirikiano kati ya Taasisi za Elimu na Waajiri, uliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Amesema Kupitia Mpango huo, sekta binafsi inaweza kuchangia maendeleo ya elimu kwa kufadhili tafiti na kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa fani mbalimbali kulingana na mahitaji ya soko la ajira.

Aidha, Makamu wa Rais ametoa wito kwa Taasisi za elimu na Sekta binafsi nchini kuzingatia maendeleo ya kasi ya sayansi na teknolojia duniani katika utekelezaji wa Mpango huo.

Amesema Vyuo na Sekta binafsi vishirikiane kubaini ujuzi muhimu unaohitajika sasa na siku zijazo hususan katika fani za sayansi, teknolojia, ubunifu, tiba, uhandisi na hesabu ili kuwezesha vijana kushindana na kupata nafasi katika soko la ajira nchini na kimataifa.

Makamu wa Rais amesema ushirikiano baina ya Taasisi za elimu na Viwandani hitaji la lazima katika dunia ya leo, kwa kuwa Vyuo haviwezi tena kuwavisiwa vya nadharia, na viwanda haviwezi kukua bila nguvukazi yenye ujuziunaoendana na teknolojia na ushindani wa soko.

Ameongeza kwamba, Serikali ya Awamu ya Sita imeweka kipaumbele chakimkakati katika kukuza ujuzi, stadi, maarifa na sifa za kuajirika au kujiajirimiongoni mwa vijana na wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu, ikitambuakwamba maendeleo endelevu ya Taifa hayawezekani bila kuwa narasilimaliwatu iliyoelimika na yenye uwezo wa kuchangia kikamilifu katikauchumi wa Taifa.

Amesema Serikali imeendelea kufanya maboresho makubwa ya sera namitaala ya elimu katika ngazi zote kwa lengo la kuujenga mfumo wa elimu uliomnyumbufu, jumuishi na unaoendana na vipaji, mwelekeo na mahitaji halisi ya soko la ajira, huku ikizingatia mabadiliko ya teknolojia na ushindani wakitaifa na kimataifa.

Uzinduzi wa Mpango huo ni utekelezaji wa ahadi ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wamwaka 2025, ambapo aliahidi kuanzisha Mpango wa pamoja kati ya Waajiri, Vyuo vya ufundi stadi na Vyuo Vikuu kwa lengo la kulinganisha mafunzo namahitaji halisi ya sekta za kipaumbele za Taifa, ndani ya siku 100 baada ya kuapishwa kwake.

Pamoja na mambo mengine, Mpango wa ushirikiano kati ya Taasisi za Elimuna Viwanda unalenga kuimarisha uhusiano wa kimkakati kati ya utoaji waelimu na utendaji kazi, kwa lengo la kulinganisha mafunzo na mahitaji yasekta za kipaumbele kama nishati, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) na viwanda vya kuongeza thamani.

Aidha, Mpango unawekamsingi thabiti wa kujenga kizazi cha wahitimu wenye uwezo wa kuajirika, kujiajiri na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa kwani umedhamiriakubadilisha mfumo wa elimu ya nadharia kwenda mfumo unaozingatia ujuzi, vitendo, ubunifu na uzalishaji mali.

Uzinduzi huo, umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Bunge, Dinipamoja na wadau wa maendeleo. Wengine waliohudhuria ni pamoja naWaajiri na Wamiliki wa Viwanda, Wakuu wa Taasisi mbalimbali, Wakuu waVyuo pamoja na Wanafunzi.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema kuwa uzinduzi wa Mpango wa Kitaifa wenye lengo la Kukuza Ujuzi na Ajira ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa Kampeni za uchaguzi kwa mwaka 2025 kwamba ndani ya siku 100 endapo atachaguliwa na kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Serikali ingeandaa na kuzindua Mpango wa kukuza ujuzi na uwezo wa kuajirika kwa vijana, na sasa ahadi hiyo imetimia kabla ya muda uliowekwa.

Prof. Mkenda ameeleza kuwa Mpango huu umeandaliwa kwa kushirikisha na wadau mbalimbali ikiwemo Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Waajiri na Wataalamu waliobobea katika kuboresha mitaala na kuongeza ujuzi akisisitiza kuwa ushirikiano huu ni msingi wa kuhakikisha Wahitimu wanapata ujuzi stahiki unaohitajika katika soko la ajira

"Yapo mafanikio tumeanza kuyaona ya ushirikino na viwanda, Wahitimu wa VETA, hususan VETA Moshi, wamekuwa wakipata ajira ndani na nje ya nchi katika maeneo kama Namibia, Guinea-Conakry, Mauritania, Kongo na Ghana hivyo uzinduzi huu utahamasisha waajiri kushirikiana zaidi, wazazi kuelewa umuhimu wa kuwapeleka watoto shuleni kupata ujuzi, na hatimaye kuchangia katika kuinua uchumi wa Tanzania," amesisitiza Prof Mkenda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akizindua Mpango wa Ushirikiano kati ya Taasisi za Elimuna Viwanda katika hafla iliyofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 09 Februari 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Ushirikiano kati ya Taasisi za Elimu na Viwanda uliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 09 Februari 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, akiwa na Viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja na baadhi ya Waajiri, mara baada ya kuzindua Mpango wa Ushirikiano kati ya Taasisi za Elimu na Viwanda katika hafla iliyofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 09 Februari 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam kwaajili ya Uzinduzi wa Mpango waUshirikiano kati ya Taasisi za Elimu na Viwanda, leo tarehe 09 Februari 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na Viongozi mbalimbali wakati akishiriki Uzinduzi waMpango wa Ushirikiano kati ya Taasisi za Elimu na Viwanda uliyofanyika katikaKituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 09 Februari 2026.

Post a Comment

0 Comments