Ticker

6/recent/ticker-posts

UWEPO WA KAMATI ZA USHAURI USHAURI NGAZI ZA KISHERIA ZITASAIDIA KUTATUA KERO ZA WANANCHI NA MALALAMIKO -RC TANGA




Na Oscar Assenga,TANGA


MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian amezindua Kamati za Ushauri wa Kisheria ngazi ya mkoa na wilaya na kliniki ya Sheria bila malipo huku akieleza kwamba zitasaidia kupunguza mashauri au migogoro dhidi ya Serikali kutokana na kukutanisha mawakili wa Serikali.

Aliyasema hayo leo kwenye viwanja vya Tangamano Jijini Tanga ambako kilifanyika uzinduzi wa Kamati hizo ambapo alisema pia wale wa taasisi mbalimbali na kuwasaidia wananchi wenye changamoto mbalimbali kupata ufumbuzi.

Alisema uwepo wa huduma hizo utawawezesha mawakili wa Serikali kusimamia utawala wa Sheria katika kushirikiana na wadau wengine katika kutatua kero za wananchi na kupunguza malalamiko ya kisheria kutoka kwa wananchi.

“Lakini pia kutoa elimu ya Sheria kwa umma katika kushughulikia changamoto mbalimbali katika maeneo yao pamoja na kutoa elimu kwa viongozi na maafisa wa Serikali waweze kutoa maamuzi kwa mujibu wa Sheria”Alisema



Aidha alisema pia itapunguza vitendo vya uonevu na vinavyovunja sheria na taratibu za nchi nah ii itawezesha mimi na wakuu wa wilaya kushughulikia masuala ya miradi ya maendeleo badala ya kuhangaika na migogoro ya wananchi .

“Lakini nanukuu katika kitabu cha Mathayo 5:9 Yesu anasema “Heri wapatanishi ,maana hao wataitwa wana wa Mungu”.Hii inaonyesha kuwa kazi ya kupatanisha ni ya Kiungu na inampendeza Mungu”

“Pia kwenye Qur’an inasititiza sana kutenda haki (Uadilifu)kama wajibu Mkuu wa kidini na kijami,ikiamrisha kusimamia haki hata kama ni dhidi ya nafsi zenu waziazi ,au jamaa (Quran 4:1:35,5.8).Uadilifu ni msingi wa imani,ukihimiza kulinda haki za wengine ,kuondoa chuki na kutoa fidia kwa wahasiriwa”Alisema

Aidha aliwataka wadau waelewe kuwa jukumu la kutatua migogoro katika maisha ya watanzania sio la Serikali pekee bali ni la wote wa maendeleo huku akieleza kazi kubwa Serikali iliyonayo ni pamoja na kutengeneza mazingira mamzuri yanayoweza kusaidia kamati hizo.

Alisema hilo linatokana na uwepo wa migogoro mingi katika jamii hasa migogoro ya ardhi na mirathi hivyo kamati hizo zinatakiwa kukaa kila mara kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake ya kusikiliza malalamiko ya ksiheria na kutoa elimu kwa umma kwa kushirikiana na ofisi za wakuu wa wilaya.

Hata hivyo alitoa rai kwamba kuna haja ya kuhakikisha kuwa kamati za mkoa na wilaya zinafanya mambo mbalimbali ili kukabiliana na migogoro ikiwemo kuendelea kuboresha kiwango cha utoaji wa huduma ya ushauri wa kisheria na kuongeza wigo na upatikanaji katika maeneo ambayo hayajafanikiwa kufikiwa hasa maeneo ya nje ya jiji.

Mkuu huyo wa mkoa alizitaka kujiwekea utaratibu wa kuandaa kliniki za kisheria bila malipo kwa utaratibu wa kuwafuata wananchi katika maeneo yaona hiyo inatokana na wapo wananchi wengine ambao wanaogopa kuingia kwenye ofisi za Serikali pamoja na wengine hawana uwezo wa kusafiri na kwenda kwenye ofisi hizo.

“Lakini hakikisheni mnapopokea malalamiko au migogoro mnaifuatilia mpaka mwisho ili kujiridhisha namna gani imemalizika na kuweka kumbukumbu ya kufungua na kufunga migogoro hii lengo likiwa kuzuia walalamikaji kurudi kuwasilisha malalamiko yaliyopita hasa pale anapoona uongozi umebadilika “Alisema

Hata hivyo nitoa wito kwa wananchi wote wa mkoa wa Tanga wenye migogoro kutumia nafasi hii kuwasilisha migogoro yenu katika kliniki ya Sheria bila malipo iliyoanza leo kwenye viwanja vya Tangamano mpaka Machi 15 mwaka huu .

Awali akzungumza akizungumza Mkurugenzi wa Uratibu na Huduma za Ushauri kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Neema Ringo alisema kwamba wamekuja mkoani Tanga kutoa huduma kwa wananchi za kisheria kwa maana yake kutekeleza wajibu wake katika kuwahudumia wananchi ambao ndio wanaipa mamlaka Serikali.

Alisema wakiwa mkoani Tanga watapata fursa ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuweza kuzipatia ufumbuzi huku akiwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo kwa kujitokeza kwa wingi kuweza kupata huduma






Post a Comment

0 Comments