Afisa Mwandamizi wa Idara ya Mahusiano kwa Jamii katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo (kulia) akipeana mkono wa shukrani na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'wale John Isack wakati wa hafla ya makabidhiano ya Trekta kwa ajili ya kusomba taka na kufanya usafi kwenye halmashauri ya Wilaya ya Nyang'wale.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'wale John Isack (kushoto) wakipongezana na Afisa Mwandamizi wa Idara ya Mahusiano kwa Jamii katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano ya Trekta kwa ajili ya usafi kwenye halmashauri ya Wilaya ya Nyang'wale.
Muonekano wa Trekta iliyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa ajili ya kusomba taka na kufanya usafi kwenye halmashauri ya Wilaya ya Nyang'wale.Viongozi wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na wa halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale wakipeana vifaa kwa ajili ya usafi kwenye halmashauri hiyo.
Afisa Mwandamizi wa Idara ya Mahusiano kwa Jamii katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena akizungumza kwenye halfa hiyo ya makabidhiano ya trekta kwa halmashauri ya Nyang’wale
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'wale John Isack (Katikati) na kulia kwake ni Senkondo Afisa Mwandamizi wa Idara ya Mahusiano kwa Jamii katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena wakiwa kwenye utiaji wa saini katika halfa ya makabidhiano ya trekta kwa ajli ya kusomba taka na ufanyaji wa usafi kwenye halmashauri hiyo
Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale wakiwa kwenye picha ya pamoja
***
Mgodi wa Barrick Bulyanhulu umeendelea kutekeleza sera yake ya mkakati endelevu wa kusaidia jamii baada ya kukabidhi trekta ya kusomba taka yenye thamani ya shilingi milioni 66 pamoja na vifaa vya kufanyia usafi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale kupitia fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) katika juhudi zake za kutunza mazingira nchini.
Akiongea katika hafla ya makabidhiano ya trekta hiyo, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Nyang'wale , Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, John Isack alisema msaada huo umekuja kwa wakati katika juhudi za kulinda na kutunza mazingira kwa maslahi ya wakazi wa wilaya hiyo na vitongoji vyake.
“Tunashukuru Barrick Bulyanhulu kwa msaada huu wa trekta , tunaamini sasa hali ya usafi katika Wilaya yetu itakuwa nzuri kwa kiasi kikubwa kwani hii ni trekta ya pili wametupatia, matarajio yetu ni kuongeza kasi ya kuondoa taka kutoka hapo awali ya kutoa mara mbili kwa wiki, awali tulikuwa tunazoa taka katika siku za Alhamisi na Jumatatu hivyo tutaongeza siku pia tunatarajia kuongeza huduma kwa maeneo ya miji inayokuwa kwa kasi kibiashara kama vile Bosolwa, Nyijundu, Bukwimba na maeneo ya migodini",alisema.
Isack aliongeza kuwa kampuni ya Barrick Bulyanhulu kupitia uwekezaji wake imefanikisha miradi mingi ya kijamii na utunzaji wa mazingira wilayani humo kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii ambayo inazidi kuboresha maisha ya wananchi.
“Leo tumepokea Trekta ambalo limenunuliwa na kampuni ya Barrick Bulyanhulu kwa gharama ya Shilingi Milioni 66 , Trekta hili ni maalum kwa kazi ya kuzoa uchafu na kupeleka dampo kwa kweli ni msaada mkubwa kwa wilaya yetu kwani kwa miaka mingi sana tumekuwa na changamoto juu ya uzoaji wa taka katika mitaa yetu ukichukulia kwamba mji wetu unakua kwa kasi na kupelekea uzalishaji wa taka kuongezeka kwa kasi, na ni matarajio yangu sasa mazingira ya Wilaya yetu yatakuwa safi, nichukue fursa hii kuwaomba wananchi kufanya usafi kila siku kwani tayari kwa sasa tunalo trekta ambalo litakuwa linasomba taka mara kwa mara”, alisema.
Kwa upande wake Afisa Mwandamizi wa Idara ya Mahusiano kwa Jamii katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo alitoa shukrani kwa viongozi wa serikali na wananchi kwa kuwa na uhusiano mzuri na Kampuni hiyo na kuongeza kuwa msaada wa trekta lililokabidhiwa ni kwa ajili ya kufanya usafi na utunzaji wa mazingira.
“Niwaombe ndugu zangu usafi ni jukumu letu sote,trekta hili tulitunze ili liweze kuboresha mazingira yetu ipasavyo ,milioni 66 ni pesa nyingi hivyo naamini tutakuwa tumefungua njia ya kuboresha mazingira ya usafi wilayani Nyang’hwale, haswa ikizingatia kampuni ya Barrick Bulyanhulu ni wadau wakubwa wa utunzaji wa mazingira”, alisisitiza Zuwena.













0 Comments