Na Paschazia Charles - Shinyanga
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Janeth Magomi, leo Jumamosi Aprili 4, 2026 wakati akizungumza na vyombo vya habari mjini Shinyanga, ambapo alieleza kuwa operesheni hizo zilianza Machi 1 hadi Machi 31, 2026 zikiwa na lengo la kukabiliana na vitendo vya uhalifu na kulinda miradi ya kimkakati.
Kamanda Magomi amesema katika operesheni hiyo, watuhumiwa hao walikamatwa katika Wilaya za Msalala na Shinyanga wakihusishwa na wizi wa vifaa hivyo.
Amesema vifaa vilivyokamatwa ni pamoja na vipande 306 vya nondo, mabomba 32 makubwa ya milimita 12, stendi za makorasha 12 pamoja na mabomba ya mraba (square pipe) 65.
Aidha, Jeshi la Polisi Tanzania kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani kiliendesha operesheni dhidi ya madereva waliokiuka sheria, ambapo baadhi walibainika kuendesha bila leseni na wengine kwa mwendo kasi uliopitiliza kilomita 80 kwa saa.
Katika ukaguzi huo, jumla ya makosa 5,648 ya barabarani yalirekodiwa, yakihusisha magari 4,044 pamoja na pikipiki na bajaji 1,604, ambapo wahusika walitozwa faini kwa mujibu wa sheria.
Kamanda Magomi ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi Tanzania kwa kutoa taarifa za uhalifu na kuzingatia usalama wao, hususan katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Pasaka.
Amesisitiza kuwa ushirikiano wa wananchi ni muhimu katika kuimarisha ulinzi wa miradi ya maendeleo na kudumisha amani katika jamii.


0 Comments