Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa ( wa nne kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa Taifa wa Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP), Dkt. Lazaro Kapella ( wa pili kulia), alipotembelea banda la mradi huo katika Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa mkoani Iringa. Picha na Kadama Malunde
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akizungumza alipotembelea Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP) katika Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa mkoani Iringa.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, ameutaja mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP) kuwa miongoni mwa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali kwa lengo la kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya maziwa nchini, kuongeza uzalishaji, kuimarisha mnyororo wa thamani wa maziwa na kuinua kipato cha wafugaji.
Waziri Bashiru amesema hayo Mei 31, 2026 alipotembelea banda la mradi huo wakati wa ufunguzi rasmi wa Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa yanayoongozwa na kauli mbiu “Rasimisha Biashara ya Maziwa Okoa Maisha ya Walaji, Ongeza Kipato, Changia Uchumi”, yanayofanyika katika Viwanja vya Mwembe Togwa mkoani Iringa, ambapo amepokea taarifa ya utekelezaji wa mradi kutoka kwa Mratibu wa Taifa wa C-SDTP, Dkt. Lazaro Kapella.
Waziri Bashiru ameagiza uongozi wa mradi kuendelea kuimarisha juhudi za kuwajengea uwezo wafugaji na wachakataji wadogo wa maziwa ili kuongeza tija katika uzalishaji, uchakataji na matumizi ya maziwa nchini.
Amesema Serikali imejipanga kuhakikisha sekta ya maziwa inakuwa mhimili muhimu wa maendeleo ya kiuchumi kwa wafugaji na Taifa kwa ujumla kupitia uwekezaji unaolenga kuongeza thamani ya mazao ya mifugo na kuboresha mazingira ya biashara ya maziwa.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akizungumza wakati wa Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa mkoani Iringa.
Aidha, Waziri Bashiru ameeleza kuwa kupitia Mradi wa C-SDTP, Serikali itaendelea kuwawezesha wafugaji kwa kuwapatia ng’ombe bora wa maziwa, kuboresha miundombinu ya ufugaji, kujenga na kukarabati vituo vya kukusanyia maziwa, kupanua masoko pamoja na kuanzisha huduma za bima ya mifugo ili kuongeza ustahimilivu wa sekta hiyo.
“Mradi huu umekusudiwa kuongeza uzalishaji wa maziwa, kuboresha mnyororo wa thamani wa maziwa na kuhakikisha mfugaji ananufaika zaidi na shughuli zake za ufugaji,” amesema Dkt. Bashiru.
Waziri huyo pia ameeleza kuwa tasnia ya maziwa nchini inaendelea kukua kwa kasi, ambapo uzalishaji wa maziwa umeongezeka kutoka lita bilioni 4.01 mwaka 2024/2025 hadi kufikia lita bilioni 4.22 mwaka 2025/2026.
Aidha, idadi ya viwanda vya kuchakata maziwa imeongezeka kutoka 156 hadi 187 katika kipindi hicho, jambo linaloonyesha kuimarika kwa uwekezaji katika sekta hiyo.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Waziri Bashiru amesema Serikali inaendelea kuhamasisha urasimishaji wa biashara ya maziwa, matumizi ya maziwa bora na salama pamoja na uwekezaji katika sekta hiyo ili kuongeza mchango wake katika uchumi wa taifa na kuboresha maisha ya wafugaji.
Ameongeza kuwa pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika uzalishaji wa maziwa, kiwango cha matumizi ya maziwa kwa Mtanzania bado ni kidogo ikilinganishwa na kiwango kinachopendekezwa kiafya, hivyo ametoa wito kwa wananchi kuongeza matumizi ya maziwa na bidhaa zake ili kuboresha afya na kusaidia ukuaji wa sekta hiyo.
Kwa upande wake, Mratibu wa Taifa wa Mradi wa C-SDTP, Dkt. Lazaro Kapella, amesema mradi huo unaendelea kuwa kichocheo muhimu cha maendeleo ya tasnia ya maziwa kwa kuwawezesha wazalishaji wadogo kushiriki kikamilifu katika mnyororo wa thamani wa maziwa, kuongeza mapato ya kaya, kuimarisha usalama wa chakula na lishe pamoja na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.
Dkt. Lazaro Kapella
Aidha Dkt. Kapella ameeleza kuwa mradi huo unatekelezwa katika mikoa nane ambayo ni Iringa, Mbeya, Morogoro, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Pwani pamoja na Zanzibar (Unguja na Pemba), ukiwa na lengo la kuongeza tija ya uzalishaji wa maziwa na kuimarisha ustahimilivu wa wafugaji dhidi ya changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
Dkt. Kapella amebainisha kuwa C-SDTP inahamasisha matumizi ya teknolojia za kisasa katika ufugaji wa ng’ombe wa maziwa, ikiwemo ufugaji wa mbari bora, upandikizaji wa mbegu kwa njia ya kisasa (Artificial Insemination), uzalishaji wa malisho bora, huduma za afya ya mifugo, pamoja na usimamizi wa samadi kwa njia rafiki kwa mazingira.
Amesema mradi huo pia unaendelea kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa matumizi ya maziwa, ubora na usalama wa maziwa pamoja na fursa zilizopo katika mnyororo mzima wa thamani wa maziwa kuanzia uzalishaji, ukusanyaji, uchakataji hadi masoko.
“C-SDTP chini ya mwongozo wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaendelea kusaidia wazalishaji wadogo wa maziwa kwa kuimarisha ushiriki wao katika mnyororo wa thamani wa maziwa, kuongeza mapato ya kaya, kuboresha usalama wa chakula na lishe pamoja na kupunguza athari za kimazingira zitokanazo na mifumo ya uzalishaji wa maziwa,” amesema Dkt. Kapella.
Ameongeza kuwa mradi huo unalenga kufanya mageuzi ya kweli katika tasnia ya maziwa kwa kuwawezesha wazalishaji wadogo kuongeza uzalishaji, kuimarisha ustahimilivu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kuboresha maisha yao kwa njia endelevu.
Mradi wa C-SDTP ni mpango wa miaka 10 (2024–2034) unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), ukiwa na lengo la kuleta mabadiliko endelevu katika sekta ya maziwa na kuboresha maisha ya jamii za vijijini.
Mradi huo unafadhiliwa na IFAD, Mfuko wa OPEC wa Maendeleo ya Kimataifa (OFID), Mfuko wa Hali ya Hewa ya Kijani (GCF) pamoja na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), huku ukitarajiwa kuwa chachu ya mageuzi makubwa katika tasnia ya maziwa nchini kwa miaka ijayo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akizungumza alipotembelea Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP) katika Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa mkoani Iringa.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akizungumza alipotembelea Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP) katika Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa yanayofanyika mkoani Iringa.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa ( wa tatu kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa Taifa wa Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP), Dkt. Lazaro Kapella (kulia), alipotembelea banda la mradi huo katika Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa mkoani Iringa.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa ( wa nne kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa Taifa wa Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP), Dkt. Lazaro Kapella ( wa pili kulia), alipotembelea banda la mradi huo katika Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa mkoani Iringa.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akizungumza wakati wa Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa yanayofanyika mkoani Iringa.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akizungumza katika Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa yanayofanyika mkoani Iringa.
Mratibu wa Taifa wa Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP), Dkt. Lazaro Kapella akizungumza katika Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa yanayofanyika mkoani Iringa.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa na wadau mbalimbali wakinywa maziwa katika Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa yanayofanyika mkoani Iringa.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akikabidhi zawadi ya cheti kwa Mratibu wa Taifa wa Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP), Dkt. Lazaro Kapella (kushoto) katika Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa yanayofanyika mkoani Iringa.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akikabidhi zawadi kwa Mratibu wa Taifa wa Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP), Dkt. Lazaro Kapella (kulia) katika Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa yanayofanyika mkoani Iringa.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga, Mhe. Emmanuel Cherehani akiwa katika banda la Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi (C-SDTP) kwenye Maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa Kitaifa mkoani Iringa.

0 Comments