Ticker

6/recent/ticker-posts

MSSPAT zaunganisha Kampuni nne kwenye madini

Na Mwandishi Wetu,Dar.

Kampuni nne za watoa huduma za bidhaa katika migodi ya madini nchini,zimeungana kwa ajili ya kufanya shughuli mbali mbali za utoaji huduma na bidhaa migodini.

Kampuni zilizoungana zipo chini ya Mwamvuli wa Umoja wa Makampuni Yanayotoa Huduma na Kusambaza Bidhaa Migodini (MSSPAT),zikiwa na umiliki wa watanzania kwa asilimia 100,huku matarajio yakiwa ni kuwa sauti moja ya kutetea maslahi yao na kuongeza ushiriki wa wazawa katika sekta hiyo.

Kampuni hizo nne zimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano chini ya katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Rotana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla ya kutia saini makubaliano hayo iliyofanyika katika hoteli ya Johari Rotana jijini Dar esSalaam, Mwenyekiti wa umoja wa Watoa Huduma na Wasambazaji wa bidhaa Migodini, Respicus Kandawa, aalisema ushirikiano huo ni muhimu kutokana na kuongezeka kwa shughuli za uchimbaji madini nchini, hali inayofungua fursa zaidi za ajira na biashara.

Alisema lengo kuu ni kuhakikisha Watanzania wananufaika ipasavyo na uwepo wa migodi, sambamba na utekelezaji wa sheria ya 'local content' inayosisitiza ushiriki wa wazawa katika utoaji wa huduma badala ya kutegemea wageni.

”Hakuna vigezo vya msingi kwa walinzi ila wamewekewa masharti magumu, ili wageni wanufaike wakati walinzi ambao wanafanya kazi ni wale walioletwa kuajiriwa na kufundishwa na wenyeji ’alisema

Aliongeza kuwa yapo makampuni ya wazawa yanyofanya kazi kwenye machimbo ila ni kwenye machimbo machache ambayo hayana masharti magumu kama yaliyowekwa maeneo mengine

“Ni muhimu sasa sisi kupewa hizo fursa ili nasi tunufaike na sekta ya madini’ alisema Mwenyekiti huyo.

Katibu wa MSSPAT, Benson Samson, akizungumza katika hiyo alisema aliwahi kufanyazi mgodini, lakini lakini alishamgazwa kuona hata bidhaa zinazopatikana hapa nchini, kama nyama, zikiagizwa kutoka nje.

Aliongeza kuwa mabadiliko ya sheria sasa yanatoa nafasi kwa wazawa kushiriki kikamilifu, hivyo kuna haja ya kuunganisha nguvu ili kuhakikisha utekelezaji wake unakuwa wa vitendo.

Alisema kuanzishwa kwa ushirikiano huo kunachochewa na utekelezaji wa sheria ya 'local content' iliyoanza kuimarishwa mwaka 2025.

Alitaja baadhi ya huduma hizo kuwa ni mazingira, bima, teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) pamoja na ulinzi.

Akizungumzia sekta ya ulinzi,Mwenyekiti wa Chama cha Ulinzi Binafsi Tanzania, Felix Kagisa, alisema licha ya kuwepo kwa walinzi zaidi ya 300,000 nchini, sekta hiyo bado inanufaisha zaidi kampuni za kigeni.

"Walinzi ni Watanzania, lakini faida inaishia kwa wageni. Sisi tunabaki kufanya kazi kupitia kampuni hizo," amesema Kagisa.

Kaimu Mkurugenzi wa Chama cha Sekta Binafsi ya Ulinzi, Kara Remtullah, amesema watatoa kipaumbele kwa vijana wa maeneo ya migodi ili wanufaike moja kwa moja na shughuli hizo.

"Tunaiomba Serikali kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sheria ili huduma hizi zitolewe na kampuni za wazawa, si kupitia mgongo wa kampuni za kigeni," amesema.

Kwa upande wake, Elly Elikana kutoka Taasisi ya Mazingira ya Green Tech Hag amesema makubaliano hayo yatafungua fursa zaidi kwa wataalamu wa mazingira wazawa kushiriki katika shughuli za migodini.

Ametoa wito kwa taasisi nyingine kushirikiana na umoja huo, huku akiitaka Serikali kuendelea kuweka mazingira rafiki yatakayowawezesha wataalamu wa ndani kunufaika na sekta ya madini.

Vyama vinne vya kisekta vilivyoingia makubaliano hayo kupitia Umoja wa Makampuni ya Watoa Huduma na Wasambazaji wa Bidhaa Migodini (MSSPAT) ni, Umoja wa Makampuni ya Washauri wa Bima na Udhibiti Majanga Tanzania (TIBA), Umoja wa Makampuni ya Ulinzi Binafsi Tanzania (TSIA),

Umoja wa Makampuni ya TEHAMA Tanzania (ICTCS) na Umoja wa Makampuni ya Washauri wa Mazingira Tanzania (GreenTech Hub).

Post a Comment

0 Comments