Meneja mkuu Balton Tanzania Jacob Vorster akishauriana na AFISA kilimo ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Innocent Keya
**
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Kampuni ya Balton Tanzania Ltd, imezindua viatilifu 10 vipya kusaidia wakulima wa Mbogamboga, Mahindi, Kahawa, Korosho,Nyanya, Vitunguu na Maharage na kukabiliana visumbufu na athari ya mabadiliko ya tabia nchi Kanda ya Ziwa.
uzinduzi wa viuatilifu hivyo,umefanyika katika viwanja vya nanenane jijini Mwanza kwa kuwashirikisha wauzaji wakubwa wa viuatilifu nchini kutoka mikoa ya Mwanza, Kigoma, Tabora, Geita, Shinyanga, Mara na Simiyu.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Balton Tanzania, Jacob Vorster akizungumza katika uzinduzi huo, amesema viuatilifu hivyo vipya ni faraja kwa wakulima wa Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla.
Alisema viiatilifu hivyo vimetengenezwa kwa teknolojia ya juu kuzuia usugu wa wadudu lakini pia kudhibiti majani ambayo hayahusiani na mazao.
Jacob aliwataka wakulima kwenda kwenye maduka ya mawakala wa pembejeo kupata viuatilifu hivyo vyenye ubora wa hali ya juu na vimeidhinishwa hapa nchini.
“Viuatilifu vyetu bora kuliko vingine sokoni na wakulima kama wanataka kupamba na visumbufu na kuwa na mavuno ya uhakika "alisema
Mtaalam wa sayansi ya mimea wa kampuni ya Balton Tanzania Chonya Wema amesema viuatilifu ni suluhisho la wadudu na athari ya mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema wakulima wa kanda ya Ziwa sasa hawana sababu ya kununua viutilifu visivyo na ubora.
"Tunajua kuna athari kubwa za mabadiliko ya tabia nchi Baltoni tumekuja na Suluhu lakini pia kuzuia magugu vamizi na wadudu wasumbufu", alisema.
Alisema timu ya mawakala imesambaa nchi nzima kuuza viuatilifu hivyo na kwa ufafanuzi zaidi umaweza kupata kwa kupiga namba 0754371202.
Afisa kilimo katika ofisi ya mkoa wa Mwanza Innocent Keya alieleza uzinduzi wa viuatilifu hivyo ni ukombozi kwa wakulima Kanda ya Ziwa.
Alisema mkoa wa mwanza umevamiwa na wadudu kantangaze ambao hawakuwahi kuwepo miaka ya nyuma na sasa suluhu imepatikana. Aliwataka mawakala wa viuatilifu kuwasaidia wakulima kununua viuatilifu vyenye ubora.
Kampuni ya Balton Tanzania inauzoefu wa usambazaji wa viuatilifu na pembejeo nyingine za kilimo kwa zaidi ya miaka 25 nchi Tanzania na nchi nyingine kadhaa barani Afrika.





0 Comments