
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndugu Rabia Abdalla Hamid , ameshiriki Mkutano Mkuu wa Chama cha Botswana National Front (BNF) unaofanyika mjini Jwaneng, Botswana, akiwakilisha Chama Cha Mapinduzi.
Akizungumza katika mkutano huo, Ndugu Rabia amesisitiza kuwa kila chama tawala kina wajibu wa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, kuimarisha misingi ya utawala bora, na kuendelea kutoa huduma zinazokidhi mahitaji ya wananchi bila kuchoka.
Aidha, amekisii Chama cha BNF kuendelea kuzingatia maslahi ya wananchi katika utekelezaji wa sera na maamuzi yake, pamoja na kuhakikisha kuwa hakuna mwananchi anayebaki nyuma katika mchakato wa maendeleo ya taifa.

Aidha,Ndg. Rabia amempongeza Rais wa Chama cha Botswana National Front (BNF) na Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mheshimiwa Duma Gideon Boko kwa ushindi wa Chama chake na kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Botswana.
Ameeleza kuwa kuchaguliwa kwa Rais Boko na Chama cha BNF ni kielelezo cha imani waliyopewa na wananchi wa Botswana na amewatakia mafanikio katika kuwaletea maendeleo na ustawi wao.
0 Comments