Ticker

6/recent/ticker-posts

MWENGE WA UHURU WATINGA TANGA, WAPITIA MIRADI 73 YA MAENDELEO

Na Mwandishi Wetu, KILINDI

MWENGE wa Uhuru 2926 umewasili katika Mkoa wa Tanga na kuanza kukagua kukagua miradi 73 ya maendeleo na huduma yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 27, ukianzia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi.

Ukiwa wilayani huo, Mwenge wa Uhuru wenye kauli mbiu inayosema ”Tanzania ni yetu sote, tushikamane kwa pamoja kuleta maendeleo” umetembelea miradi saba yenye thamani ya jumla ya Shilingi 863,671,832.37.

Miradi hiyo ni ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Kwekivu, kivuko cha Mapanga, zanahati binafsi ya Kite iliyopo kijiji cha Mafulila, mradi wa maji katika Kijiji cha Ludewa, vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja katika Shule ya Sekondari Kikunde, nyumba ya kulala wageni ya JS Sembela na kikundi cha vijana Waloti kilichopo Kikunde.

Kwenye hafla ya mapokezi, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian aliyekabidhiwa Mwenge na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, alisema Mwenge huo utakimbizwa kwa umbali wa kilomita 1,340 kupitia Halmashauri zote 11 za Mkoa wa Tanga.

Alisema, katika siku 11 utakaokuwepo mkoani Tanga, Mwenge wa Uhuru utaendelea kuhamasisha maendeleo, uwajibikaji na ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo.

Mhe. Balozi Dkt. Batilda alisema, miradi inayopitiwa na Mwenge ni sehemu ya miradi mingi iliyopo kwenye sekta za elimu, afya, maji, miundombinu na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi, inayolenga kuboresha maisha na huduma kwa wananchi mkoani humo.

Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwang’onda, alitumia mbio hizo kuwahimiza wananchi kuendelea kutunza amani, umoja na mshikamano, akivitaja kuwa ni sehemu ya nyenzo zenye kuweka mazingira kufanikisha maendeleo nchini.

Pia, Mwang’onda, amewahimiza wakazi wanaoishi kwenye maeneo ya karibu na yanayozunguka miradi na huduma kwa jamii, kuwa walinzi wa rasilimali hizo na nyingine za umma, zinazochochea ustawi na maendeleo.

Post a Comment

0 Comments