Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) linashiriki Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) kwa kuanzisha Kijiji cha Mazingira, jukwaa maalum linalowakutanisha wananchi, wadau wa mazingira na taasisi mbalimbali kwa lengo la kutoa elimu, kuonesha ubunifu na teknolojia rafiki kwa mazingira, pamoja na kuhamasisha uhifadhi na usimamizi endelevu wa mazingira.
Kijiji cha Mazingira kimekuwa kivutio kwa wageni wanaotembelea maonesho hayo, ambapo wanapata elimu kuhusu usimamizi wa taka, urejelezaji, uhifadhi wa bioanuwai, matumizi ya teknolojia rafiki kwa mazingira na utekelezaji wa sheria za mazingira.
Aidha, wataalamu kutoka NEMC pamoja na wadau mbalimbali waliopo ndani ya Kijiji cha Mazingira wanatoa ushauri wa kitaalamu na kujibu maswali ya wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya mazingira.
NEMC inawakaribisha wananchi wote kutembelea Kijiji cha Mazingira kilichopo katika viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) ili kujifunza, kupata huduma za ushauri wa kitaalamu, kushuhudia ubunifu wa wadau wa mazingira na kushiriki kikamilifu katika juhudi za kuhifadhi mazingira kwa maendeleo endelevu ya Taifa na ustawi wa vizazi vya sasa na vijavyo.









0 Comments