Mkuu wa Polisi wilaya ya Kipolisi Mbagala Mrakibu wa Polisi SP Neema Makyao akiwa ameambatana na Mkuu wa Polisi Jamii wa wilaya hiyo Mrakibu wa Polisi SP Tatu Mayugi pamoja na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali wamefanya usafi katika maeneo ya Soko la Matunda Mbagala Rangi tatu Julai 23,2026.
SP Neema amesema matendo hayo ni ya kawaida kwa Jeshi hilo ili kuweka mazingira safi na kulinda Afya dhidi ya magonjwa ya mlipuko na hayo pia ni katika shamra shamra za kuelekea kilele cha siku ya Polisi Jamii ambayo itafanyika Tarehe 25,2026, sambamba na hayo kumekuwa na matendo ya Huruma na shughuri mbalimbali kuhanikiza kilele cha siku hyo.
Naye Mkuu wa Polisi Jamii wa Wilaya hiyo Mrakibu wa Polisi SP Tatu Mayugi amewashukuru Wananchi, wafanya Biashara na madereva wa Eneo hilo kwa kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi hilo pia amewataka kutojihusisha na vitendo vya kihalifu badala yake wawe mstari wa mbele kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuweza kuweka maeneo yao katika hali ya ushwari wa Kiusalama.
Aidha Ndugu Hamidu Hemed ambae ni mfanya Biashara mdogo wa Soko hilo la matunda ameshukuru kwa Ujio huo na amewataka wawe wanafanya hivyo mala kwa mala ili wadumishe mahusiano kati yao na Jamii kwa ujumla.






0 Comments