Ticker

6/recent/ticker-posts

ULINZI SHIRIKISHI NI MSINGI WA AMANI NA USALAMA.

Na Issa Mwadangala.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe amewashukuru wananchi wa Kijiji cha Maleza Kata ya Mbangala Wilaya na Mkoa wa Songwe kwa kuendelea kudumisha hali ya usalama na amani, akibainisha kuwa kata hiyo imeendelea kuwa tulivu na haina changamoto kubwa za uhalifu kama zilivyo katika baadhi ya maeneo mengine.

Ameyasema hayo Julai 24, 2026 akiwa katika ziara ya Serikali nyumbani kwako katika kata hiyo na kuwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kwa kutoa taarifa za uhalifu au watu wanaowatia shaka mara wanapobaini mienendo isiyo ya kawaida.

"Ulinzi na usalama huanza kwa wananchi wenyewe kupitia dhana ya ulinzi shirikishi na ulinzi wa jirani mnaweza kutoa taarifa zinaweza kutolewa kwa viongozi wengine wa kata ili ziweze kufikishwa na kufanyiwa kazi na mnatakiwa kukemea vitendo viovu vinavyoharibu maadili ya watoto na vijana, kwani ndiyo viongozi wa baadae na wanapaswa kulelewa katika mazingira yenye maadili mema" alisema Kamanda Senga.

Mwisho, Kamanda Senga alisema kile ambacho hupendi kutendewa, usimtendee mwenzako, huku akieleza kuwa migogoro, chuki na vitendo vya ukatili hujenga mazingira ya mashaka, imani potofu za ushirikina na hata kusababisha matukio ya mauaji, huku akiwataka waendelee kushikamana, kulinda vijiji vyao na kufanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii kwa amani, utulivu na usalama.

Post a Comment

0 Comments