Ticker

6/recent/ticker-posts

VIONGOZI NA WATUMISHI WA TRA WASIMAMA NA KUPIGA MAKOFI KWA DAKIKA 1 KUWASHUKURU WALIPAKODI

  

Viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamesimama na kupiga makofi kwa muda wa dakika moja wakati wa kikao cha tathmini ya utendaji kazi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ikiwa ni ishara ya kuwapongeza na kuwashukuru Walipakodi kote nchini kwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari.

Wakati wa tukio hilo jijini Arusha Julai 06, 2026 ambalo pia lilishuhudiwa na baadhi ya walipakodi waliofika kwenye ukumbi wa mikutano wa AICC kwa mwaliko wa Kamishna Mkuu wa TRA, ameeleza kwamba Mamlaka hiyo inathamini sana mchango wa Walipakodi wote nchini maana bila wao mafanikio yaliyopo yasingepatikana.

"Tunatambua na kuthamini mchango wa Walipakodi wa thamani wa nchini, maana ndiyo wameiwezesha TRA kupiga hatua, bila ninyi tusingezungumza haya mafanikio makubwa tuliyoyapata na hii ndiyo sababu ya kusimama na kupiga makofi (Standing Ovation) kwa muda wa dadika moja" amesema Bw. Mwenda.

Kamishna Mkuu Mwenda amesema inapozungumzwa miaka 30 ya TRA haiwezi kutanjwa bila kuwahusisha wafanyabiashara na kuwaahidi kuwa TRA itaendelea kuwapatia huduma bora za Kodi.

Aidha Kamishna Mkuu Mwenda amesema katika kikao hicho cha tathmini ya utendaji kazi, wataweka mikakati ya kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya TRA huku akiweka wazi namna makusanyo ya kodi yalivyoongezeka kutoka Sh. Trilioni 21 kwa mwaka wakati Rais anaingia madarakani hadi kufikia Sh. Trilioni 37.96 kwa mwaka hivi sasa.

Post a Comment

0 Comments