Ticker

6/recent/ticker-posts

KAIRUKI: TTCL ISIPIME FAIBA KWA HOME PASS PEKEE



Na Mwandishi Wetu - DAR ES SALAAM


Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, ameitaka TTCL kubadilisha mtazamo wa kupima mafanikio ya huduma ya Faiba Mlangoni Kwako, akisema idadi ya Home Pass pekee haitoshi kuthibitisha mafanikio ya mradi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Awamu ya Pili ya mradi huo jijini Dar es Salaam, Waziri Kairuki amesema mafanikio yanapaswa kupimwa kwa kuangalia idadi ya wateja wanaounganishwa, ubora wa huduma, kasi ya intaneti na kiwango cha kuridhika kwa wateja.


Ametaka TTCL pia kuimarisha huduma kwa wateja na kuhakikisha malalamiko yanashughulikiwa kwa haraka na kwa ufanisi.

Amesisitiza kuwa huduma hiyo inapaswa kufika maeneo yenye mahitaji makubwa, yakiwemo makazi mapya, masoko, biashara, viwanda, shule, vyuo, vituo vya afya na ofisi za Serikali.


Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, CPA Moremi Marwa, amesema Awamu ya Pili inalenga kuongeza zaidi ya Home Pass 400,000, huku Shirika likitumia teknolojia ya GPON.

Marwa amesema Awamu ya Kwanza tayari imewezesha TTCL kujenga zaidi ya 280,000 Home Pass na kufikisha karibu 300,000 maungio ya fibre.

Waziri Kairuki amesema ubora na affordability ya huduma ni muhimu ili wananchi wanufaike kikamilifu na uwekezaji unaofanyika katika miundombinu ya mawasiliano.





Post a Comment

0 Comments