Ticker

6/recent/ticker-posts

KATIBU MKUU CCM AONGOZA KIKAO CHA SEKRETERIETI YA HALMASHAURI KUU YA CCM






Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, akiongoza Kikao cha Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, wakati wa kuwapokea na kuwatambulisha wajumbe walioteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), hivi karibuni. Katika kikao hicho kilichofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam, leo Jumamosi, tarehe 1 Agosti 2026, pia Balozi Dkt. Migiro alishuhudia makabidhiano ya ofisi na majukumu kati ya viongozi wapya na wanaoondoka

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndugu Aggrey Mwanri akipokewa na kusalimiana kwa tabasamu na bashasha na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Ndugu John Mongella, leo Jumamosi, tarehe 1 Agosti 2026, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam, wakati wa mapokezi ya Wajumbe wa Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, walioteuliwa hivi karibuni.



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro (katikati) akishuhudia makabidhiano ya ofisi na majukumu, kati ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Komredi Aggrey Mwanri (kushoto pichani) na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Komredi John Mongella (kulia pichani), yaliyofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar Es Salaam, leo Jumamosi, tarehe 1 Agosti 2026.


Post a Comment

0 Comments