Ticker

6/recent/ticker-posts

ONJA LEO POMBE HII YA MITISHAMBA UONE UPEKEE!

 

Dar es Salaam | 31 Julai 2026

Kwa wiki kadhaa, swali moja limekuwa likiulizwa kila sehemu—mitandaoni, kwenye WhatsApp, hata pale unapokutana na marafiki kwenye baa.

Watu wamekuwa wakiuliza: "Kwa nini mitishamba inazungumzwa sana hivi karibuni?"

Wengine walidhani ni dawa mpya. Wengine walisema labda ni filamu. Wengi hawakujua.

Sasa jibu limefika.

Serengeti Breweries Limited imezindua ORIJIN. Ni pombe, lakini pombe inayotokana na mitishamba ya Kiafrika—herbs, roots na fruits ambazo Watanzania wamekua nazo, ambazo bibi zetu walizungumza nazo.

Kabla ORIJIN haijafahamika, kampeni ya ORIJINO MITISHAMBA ilikuwa imeshaanzisha mazungumzo. Watu walishiriki uzoefu wao. Wengine wakasimulia hadithi za bibi zao. Wengine wakielezea jinsi mitishamba ilivyowasaidia. Wengine wakibishana kuhusu nini ina nguvu kuliko nini.

Lakini hakuna aliyefahamu kwamba yote yalikuwa yakipelekea kitu.

Siri ilikuwa inajengwa. Na leo, imefichuliwa.

ORIJIN inaleta ladha ya uchungu na utamu, kama mitishamba mingi unayoijua, lakini kwa mfumo wa kisasa. Imetengenezwa na SBL, ikitumia viwango vya Diageo.

Inapatikana katika aina mbili:

👉RTD — tayari kunywa

👉Bitters — kwa wale wanaopenda ladha tamu yenye uchungu

Dar es Salaam ndio mji ulioshuhudia uzinduzi. Wageni walionja ORIJIN mara ya kwanza.

Media, creators na washirika wa sekta walikuwepo.

Wengi walisema inawakumbusha vinywaji vya kitamaduni, lakini kwa mtindo wa kisasa.

Wengine waliuliza: "Mbona haikuja mapema?"

Wanasema wanataka Watanzania wapate kinywaji kinachowagusa, kinachowawakilisha. Si pombe tu. Ni heshima kwa mitishamba ya Kiafrika.

Baada ya wiki kadhaa, jibu limefahamika. ORIJIN ipo sokoni.

Swali sasa ni: Wewe utaionja?

Post a Comment

0 Comments