Ticker

6/recent/ticker-posts

WIZARA YA MAJI YAWASILISHA MPANGO WA GRIDi YA TAIFA YA MAJI KWA KAMATI YA BUNGE

Wizara ya Maji imewasilisha taarifa ya utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa Gridi ya Taifa ya Maji kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira.

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (Mb) akiwasilisha taarifa hiyo kwa niaba ya Waziri wa Maji amesema utekelezaji huo ulishaanza kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maji ambayo inatumia vyanzo vya uhakika vya Maji ikiwemo mradi wa maji ya ziwa Victoria ambayo yamefika Shinyanga hadi wilaya za mkoa wa Tabora na kazi ikiendelea kufikisha maji Dodoma.

Amesema Gridi ya Taifa ya Maji ambayo ni kichocheo kikubwa cha kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya 2050 unatarajiwa kuwa na mtandao wenye urefu wa zaidi ya Km 6200 ambao utahusisha mitaro ya wazi zaidi ya Km 1200 na mabomba zaidi ya Km 5000.

Mradi huo utatekelezwa kwa awamu tatu hadi kukamilika kwake mwaka 2050.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Jackson Kiswaga (Mb) amepongeza na kutaka uzingatiaji wa mahitaji yote ya maji kwa matumizi ya nyumbani, mifugo na mimea.

Post a Comment

0 Comments