Fidele, rapper mwenye asili ya Congo aliyekulia nchini Malawi na kwa sasa anaishi Australia, anaendelea kujenga jina lake kupitia muziki unaochanganya ushairi, simulizi na mizizi ya Kiafrika.
Safari yake ya muziki ilianza akiwa na miaka 17, baada ya mwalimu wake wa kidato cha kwanza kumpa kazi ya kuandika shairi kuhusu elimu kama ufunguo wa mafanikio. Badala ya shairi hilo kubaki darasani, Fidele alilibadilisha kuwa wimbo, na hapo ndipo safari yake ya muziki ilipoanzia.
Akiwa mwandishi wa nyimbo na rapper, Fidele hutumia maneno kusimulia hisia, maisha na uzoefu wake. Mchanganyiko wa asili yake ya Kiafrika na maisha yake ya Australia unampa mtazamo wa kipekee katika muziki wake.
Kwa sasa, Fidele ameachia wimbo wake mpya uitwao “Letter to Louise,” unaoendelea kuonyesha upande wake wa kisanii kupitia uandishi wenye mguso wa kishairi na simulizi binafsi.
Fidele, ambaye analenga kufikisha muziki wake kwenye hadhira ya kimataifa, pia yuko wazi kwa ushirikiano na lebo za muziki zinazoweza kusaidia kukuza safari yake ya kisanii.
“Letter to Louise” ni hatua nyingine katika safari ya Fidele kutoka kwenye shairi la darasani hadi kwenye ndoto ya kufika kwenye jukwaa la kimataifa.
Tazama Video hii hapa



0 Comments