Na; Mwandishi Wetu- Dar es Salaam
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonazi ameongoza Kikao cha Makatibu Wakuu kutoka katika Wizara zinazotekeleza Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP), Wakuu wa Taasisi pamoja na Wakurugenzi wa Sekta, pamoja na wataalam kutoka katika sekta hizo na Ujumbe Kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Mtaa wa Magogoni Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Septemba 2026.
Kikao hicho kimefanyika baada ya ziara maalumu ya wataalamu kutoka IFAD na AFDP kukamilisha ziara ya kutembelea maeneo yanayotekeleza Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi ya kupima matokeo utekelezaji wa program ya muda wa kati (MTR)
Pamoja na mambo mengine IFAD wamepongeza Serikali kwa Kusimamia vyema Shughuli za Programu kwa kuleta matokeo chanya kwa wananchi..Aidha kikao hicho kimepokea wasilisho la dondoo lnayoainisha hoja za makubaliano yaliyopendekezwa kuhusiana na mwenendo wa utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP).



0 Comments