Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

TAIFA GAS YAENDESHA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA UJAZAJI NA USAMBAZAJI WA GESI HARAMU MKOA WA DAR ES SALAAM

 

Meneja Mauzo wa Mkoa wa Dar es Salaam wa Taifa Gas, Enock Ngulwa , akitoa maelezo na ufafanuzi ya jinsi ya matumizi sahihi ya gesi kwenye semina ya siku moja kwa wawakilishi wa Umoja wa Ulinzi Shirikishi Tanzania (USHITA) kwa Mkoa wa Dar es Salaam
Meneja Mauzo wa Mkoa wa Dar es Salaam wa Taifa Gas, Enock Ngulwa , akitoa maelezo na ufafanuzi ya jinsi ya matumizi sahihi ya gesi kwenye semina ya siku moja kwa wawakilishi wa Umoja wa Ulinzi Shirikishi Tanzania (USHITA) kwa Mkoa wa Dar es Salaam 
Meneja Mauzo wa Taifa Gas Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Joseph Richard (kulia) akikabidhi cheti kwa mmoja wa washiriki wa mafunzo.
Washiriki wa mafunzo wakionesha vyeti vyao baada ya kukamilisha mafunzo ya matumizi sahihi ya gesi na udhibiti wa ujazaji haramu wa gesi.
Washiriki wa mafunzo wakionesha vyeti vyao baada ya kukamilisha mafunzo ya matumizi sahihi ya gesi na udhibiti wa ujazaji haramu wa gesi.
Washiriki wa mafunzo ya Taifa Gas na wawakilishi wa USHITA wakipiga picha ya pamoja baada ya kukamilisha mafunzo.
****
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya Taifa Gas imefanya mafunzo ya siku moja ya elimu kwa wawakilishi wa Umoja wa Ulinzi Shirikishi Tanzania (USHITA) juu ya matumizi sahihi ya mitungi ya gesi na Ujazaji haramu wa gesi (Illegal Refill) katika jitihada za kuongeza uelewa kwa jamii na kupambana na tatizo hilo nchini.

Akizungumza wakati wa mafunzo haya jijini Dar es Salaam Septemba 19,2026 , Meneja Mauzo wa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani , Joseph Richard amesema kwamba mafunzo yamelenga kuwajengea uelewa kwa kada hiyo ya ulinzi shirikishi ili kuweza kuongeza kasi ya mapambano ya udhibiti wa ujazaji haramu na usambazaji wa gesi bila vibali mitaani.

“Mafunzo hayo pamoja na mambo mengine wawakilishi hawa wa ulinzi shirikishi wamepata fursa ya kujifunza kuhusu matumizi ya gesi , jinsi ya kudhibiti gesi wakati inataka kulipuka na utunzaji wa mazingira,’ amesema Richard.

Aliongeza kuwa semina hiyo pia imelenga kuwafundisha jinsi ya kutumia gesi kwa usahihi na kulinda usalama kwenye maeneo wanapoishi pamoja na kuwabaini watu wanaojihusisha na ujazaji na usambazaji wa gesi haramu ambayo haijathibitishwa na mamlaka husika.

 Richard ambaye anasimamia mauzo ya Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani aliongeza kwamba wameamua kuwashirikisha kada hiyo kwa sababu ya kudumisha usalama na kuchukua hatua kwa haraka pale wanapobaini kuna viashiria vya ujazaji na usambazaji wa gesi haramu kwenye maeneo wanapoishi.

“Mafunzo haya yamefanyika kwa takribani wawakilishi 26 wa Mkoa wa Dar es Salaam kutoka kwenye Umoja huu wa Ulinzi Shirikishi Tanzania (USHITA) ili kupanua wigo wa uelewa wa mambo ya ujazaji haramu wa gesi na kuongeza kasi ya mapamabano ya biashara hiyo haramu ili kulinda usalama wa raia na mali zao,” alisisitiza.

Alifafanua kuwa mafunzo hayo yameanza kwenye Mkoa wa Dar es Salaam ila mipango inaendelea kuhakikisha mafunzo hayo pia yanafanyika kwenye Mikoa na majiji ya Mwanza, Arusha, Tanga , Dodoma na Morogoro ili elimu ya matumizi sahihi ya mitungi ya gesi na jinsi ya kudhibiti ujazaji haramu na usambazaji za gesi kinyume cha sheria za nchini ianze kusambaza kwenye maeneo mengine.

Kwa upande wake , Maxwell Masuba Mhandisi wa Taifa Gas alisema mafunzo hayo pia yalilenga jinsi ya kuwafudisha madhara ya uchakachuaji wa gesi na uharibifu wa mazingira na jinsi jamii inavyohatarisha maisha yao kwenye biashara hiyo haramu.

“Kuna madhara makubwa sana kwenye uchakachauji wa gesi kutoka mtungi moja hadi mwingine jinsi ya usambazaji wake unavyoweza kuhatarisha maisha ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla,” aliongeza

Alisema kwamba ujazaji haramu wa gesi na usambazaji mara nyingi wanatumia vifaa visivyo sahihi katika ujazaji na usambazaji wa gesi hiyo unatoka kwenye mitaa na siyo kwenye kituo cha kampuni (Depot).

Aliongeza kwamba ni muhimu kwa jamii wa watanzania kuelewa jinsi ya kutumia gesi kwa usahihi , jinsi ya kupambana na matumizi ya usambazaji wa gesi haramu mitaani na kujua jinsi ya kuzima gesi pindi inapotaka kulipuka kwa ajili ya usalama wao.

Enock Ngulwa , Meneja Mauzo wa Mkoa wa Dar es Salaam wa Taifa Gas alisema kwamba wawakilishi hao wa Umoja wa Ulinzi Shirikishi (USHITA) watakuwa mabalozi ya jinsi ya kukabiliana na wimbi la ujazaji wa gesi haramu mitaani.

Alisisitiza kwamba kufanya biashara ya ujazaji na usambazaji wa gesi bila vibali unaleta hasara kwa taifa na kupunguza mapato ya serikali kwahiyo kampuni hiyo imechukua jukumu la kutoa mafunzo ya matumizi sahihi ya gesi na kujenga uelewa wa ujazaji na usambazaji wa gesi haramu nchini.

Msafiri Hamisi Mlinzi shirikishi kutoka Kinondoni alisema kwamba mafunzo hayo ni muhimu kwao kwa sababu wao ni sehemu ya usalama wa jamii ni muhimu kujua matumizi ya gesi kwa usahihi na ujazaji wa gesi haramu kwenye mitaa ili waweze kukabiliana na tatizo hilo.

“Kwetu sisi ni wakati muafaka kwa kuweza kujifunza na namna bora ya kukabiliana na tatizo hilo la biashara haramu ya ujazaji wa gesi mitaani bila vibali ili tuweze kushirikiana na Taifa Gas katika kuwakatamata na kuwafikisha kwenye vyombo ya sheria,” amesema Hamisi.

Naye Faraji Rashid Kiluwa kutoka Bunju alisema kwamba mafunzo hayo ni muhimu kwao kwa sababu wamejifunza matumizi ya nishati hiyo safi ya gesi na kukabiliana na majanga kama ya moto wakati gesi inapolipuka.












Post a Comment

0 Comments