-Akutana na kufanya mazungumzo na katibu mkuu wa viwanda. Biashara na Uwekezaji wa Oman;
-Asema mauzo ya bidhaa za Tanzania nchini Oman yaongezeka
Zanzibar
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Balozi Waziri Salum amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji kutoka nchini Oman Mhe. Ibtisam Al Farooji na ujumbe wake wenye lengo la kudumisha ushirikiano wa kiuchuni na kibiashara kati ya nchi hizi mbili.
Balozi Waziri aliueleza ujumbe wa Katibu Mkuu huyo juu ya fursa za biashara zilizoko hapa Nchini na nia ya Tanzania kuongeza mauzo ya bidhaa zake Nchini Oman hususani kwenye soko la mifugo na bidhaa za kilimo
Alisema mauzo ya biashara kati Tanzania na Oman yameongezeka kutoka dola milioni 18 mwaka 2017 hadi kufikia dola milioni 160.8 mwaka 2025 huku Tanzania ikiagiza bidhaa za mafuta na gesi kutoka nchini Oman.
Tanzania na Oman zimekuwa na ushirikiano mkubwa wa kibiashara wenye kubeba historia ya muda mrefu.





0 Comments