Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA) Sheha Mjaja Juma akizungumza na Wataalamu na Watafiti kutoka Wizara, Taasisi za Umma na sekta binafsi wakati wa ufunguzi wa kikao kuhusu maandalizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi kuhusu Usimamizi wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi. Kikao hicho kimefanyika Septemba 15, 2026 Unguja, Zanzibar.
************
Wataalamu na watafiti kutoka Wizara, Taasisi za Umma na sekta binafsi wamehimizwa kubainisha vipaumbele vya kimkakati ili kuhakikisha Tanzania inanufaika vyema na Mkutano wa 12 wa Mkataba wa Nairobi unaotarajia kufanyika nchini kuanzia tarehe 6-9 Oktoba, mwaka huu.
Hayo yamesemwa Septemba 15, 2026 Mjini Zanzibar na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA) Sheha Mjaja Juma wakati akifungua kikao cha wataalamu kuhusu Maandalizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi (COP 12).
Mjaja amesema Mkutano wa COP 12 unafanyika katika kipindi muhimu ambapo Tanzania Bara na Zanzibar zinatekeleza ajenda za maendeleo za muda mrefdu kupitia Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050 na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
“Dira hizi zinatambua umuhimu wa matumizi endelevu ya rasilimali za asili, ulinzi wa mazingira na kujenga uchumi unaostahimili mabadiliko ya tabianchi, hivyo ni fursa muhimu kuainisha mijadala ya kikanda na mikakati ya uchumi wa buluu” amesema Mjaja.
Kwa mujibu wa Mjaja amewataka wataalamu hao kuhakikisha changamoto kuhusiana na uchafuzi wa bahari, taka za plastiki, uharibifu wa matumbawe, uvuvi usio endelevu zinapata majibu ya pamoja na kuweza kufanyiwa kazi.
Mjaja amebainisha masuala muhimu ya wataalamu hao yanayopaswa kuzingatiwa ni mbinu za kuimarisha uchumi wa buluu endelevu, uhifadhi wa mifumo ikolojia ikiwemo mikoko, matumbawe na maeneo oevu.
Amesema afya ya bahari na ukanda wa pwani ni msingi wa afya ya jamii, usalama wa chakula, ajira, kipato na ustawi wa wananchi ambao unabeba mustakabali endelevu wa maisha na ustawi wa jamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Paul Deogratius amesema malengo ya mkutano huo ni pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji wa Mkataba wa Nairobi na pamoja na kupokea taarifa ya mapato na matumizi ya fedha.
Dkt. Paul piua amebainisha manufaa ya Mkutano wa COP 12 ni pamoja na kuiwezesha Tanzania kuimarisha diplomasia ya mazingira katika majukwaa ya kikanda na kimataifa, kuvutia uwekezaji katika sekta za uvuvi, utalii, nishati na usafiri.
“Tanzania imeendelea kuweka mkazo katika masuala ya uhifadhi wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi sambamba na matumizi endelevu ya rasilimali na kukuza uchumi wa Buluu” amesema Dkt. Deogratius.
Naye Mkuu wa Sekretarieti ya Mkataba wa Nairobi, Dkt. Jaredi Bosire ameipongeza maandalizi ya Serikali ya Tanzania kuelekea Mkutano wa COP 12 na kuzitaka Nchi wanachama kuiga mfano huo kuelekea mikutano ijayo.
Amesema mkutano wa COP 12 umeweza kuvutia idadi kubwa ya washiriki ambapo hadi kufikia sasa jumla ya washiriki 800 wameweza kujisajili katika tovuti ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP).
Dkt. Bosire amesema katika Mkutano huo pia umepanga kuwa na jumla ya mikutano ya pembezoni takribani 50 ikilinganisha na mikutano 40 ya aina hiyo iliyofanyika katika mkutano uliofanyika Madagascar mwaka 2024.
Mkataba wa Nairobi kuhusu Usimamizi na Uendelezaji wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi unatekelezwa na Nchi Wanachama 10 ambazo ni Tanzania, Komoro, Kenya, Somalia, Madagascar, Mauritius, Msumbiji, Shelisheli na Ufaransa.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Paul Deogratius akizungumza na Wataalamu na Watafiti kutoka Wizara, Taasisi za Umma na sekta binafsi wakati wa ufunguzi wa kikao kuhusu maandalizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi kuhusu Usimamizi wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi. Kikao hicho kimefanyika Septemba 15, 2026 Unguja, Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Uchumi wa Buluu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Magdalena Ngotolainyo akizungumza na Wataalamu na Watafiti kutoka Wizara, Taasisi za Umma na sekta binafsi wakati wa ufunguzi wa kikao kuhusu maandalizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi kuhusu Usimamizi wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi. Kikao hicho kimefanyika Septemba 15, 2026 Unguja, Zanzibar.
Wakili Mkuu wa Serikali Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Bi. Vaileth Machary akizungumza jambo wakati wa kikao cha Wataalamu na Watafiti kutoka Wizara, Taasisi za Umma na sekta binafsi kuhusu maandalizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi kuhusu Usimamizi wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi. Kikao hicho kimefanyika Septemba 15, 2026 Unguja, Zanzibar.
Mratibu wa Mipango ya Bahari kutoka Shirika la Uhifadhi wa Maizngira Duniani (WWF) Dkt. Modesta Medard akizungumza jambo wakati wa kikao cha Wataalamu na Watafiti kutoka Wizara, Taasisi za Umma na sekta binafsi kuhusu maandalizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi kuhusu Usimamizi wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi. Kikao hicho kimefanyika Septemba 15, 2026 Unguja, Zanzibar.
Maafisa Waandamizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Bi. Salome Musangile na Bi. Vaileth Machary wakijadialiana jambo wakati wa wa kikao cha Wataalamu na Watafiti kutoka Wizara, Taasisi za Umma na sekta binafsi kuhusu maandalizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi kuhusu Usimamizi wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi. Kikao hicho kimefanyika Septemba 15, 2026 Unguja, Zanzibar.
Afisa Takwimu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Bi. Caroline Gweso akizungumza jambo wakati wa kikao cha Wataalamu na Watafiti kutoka Wizara, Taasisi za Umma na sekta binafsi kuhusu maandalizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi kuhusu Usimamizi wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi. Kikao hicho kimefanyika Septemba 15, 2026 Unguja, Zanzibar.
Watendaji Waandamizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Bi. Sophia Kivina na Zahara Suleiman wakifuatilia kikao cha Wataalamu na Watafiti kutoka Wizara, Taasisi za Umma na sekta binafsi kuhusu maandalizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi kuhusu Usimamizi wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi. Kikao hicho kimefanyika Septemba 15, 2026 Unguja, Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA) Sheha Mjaja Juma (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar muda mfupi baada ya kufungua kikao cha Watalaamu na Watafiti kutoka Wizara, Taasisi za Umma na sekta binafsi kuhusu maandalizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkataba wa Nairobi kuhusu Usimamizi wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi. Kikao hicho kimefanyika Septemba 15, 2026 Unguja, Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA) Sheha Mjaja Juma (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar muda mfupi baada ya kufungua kikao cha Watalaamu na Watafiti kutoka Wizara, Taasisi za Umma na sekta binafsi kuhusu maandalizi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuelekea Mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama Zinazotekeleza Mkatab awa Nairobi kuhusu Usimamizi wa Mazingira ya Bahari na Ukanda wa Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi. Kikao hicho kimefanyika Septemba 15, 2026 Unguja, Zanzibar.










0 Comments