Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Responsive Advertisement

NSSF YAPUNGUZA MUDA WA MALIPO YA MAFAO, WANACHAMA WAHIMIZWA KUTUMIA NSSF PORTAL

Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi, akizungumza Oktoba 5,2026 wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 yaliyofanyika katika Ofisi za NSSF Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi, akizungumza Oktoba 5,2026 wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 yaliyofanyika katika Ofisi za NSSF Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde
Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi, akizungumza Oktoba 5,2026 wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 yaliyofanyika katika Ofisi za NSSF Mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Shinyanga

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umewataka wanachama wake kutumia kikamilifu huduma za kidijitali za Mfuko, hususan kufungua na kufuatilia madai ya mafao kwa njia ya mtandao, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma, kuokoa muda na kupunguza ulazima wa kufika katika ofisi za NSSF.

Wito huo umetolewa Oktoba 5, 2026 na Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi wakati akifungua maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 katika Ofisi za NSSF Shinyanga, yenye kaulimbiu “Huduma Bora kwa Vitendo.”

Amesema NSSF imeendelea kuimarisha matumizi ya teknolojia katika kuboresha huduma kwa wanachama, waajiri na wastaafu.

Mdabi amesema kupitia Lango la Huduma za NSSF (NSSF Portal), wanachama wanaweza kujisajili, kufuatilia taarifa za michango, kufungua na kufuatilia madai ya mafao pamoja na kupata huduma nyingine bila kulazimika kufika katika ofisi za Mfuko. 

Amesema matumizi ya mifumo hiyo yameendelea kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma na ulipaji wa mafao.

Amesema maboresho hayo yamewezesha wastani wa muda wa kulipa mafao kupungua kutoka siku 63 katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 2021 hadi siku 19 katika mwaka wa fedha 2025/2026, akisisitiza kuwa wanachama wanapaswa kutumia fursa za kidijitali ili kupata huduma kwa haraka na kwa urahisi zaidi.

Aidha, Mdabi amewataka wanachama kuendelea kufuatilia taarifa zao za NSSF na kutoa taarifa kwa Mfuko pale wanapobaini changamoto au kutokuwapo kwa michango yao. 

Amesema hatua hiyo ni muhimu katika kuhakikisha taarifa zao zinakuwa sahihi na kulinda haki zao za kupata mafao kwa wakati.

Kwa upande mwingine, amesema NSSF imeendelea kupanua wigo wa Hifadhi ya Jamii kwa kuwafikia wananchi waliojiajiri na wanaofanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Hadi Juni 30, 2026, idadi ya wanachama ilifikia 2,144,906, kutoka 1,616,026 Juni 30, 2025, sawa na ongezeko la asilimia 33, huku thamani ya Mfuko ikifikia Shilingi trilioni 11.4.

Mdabi amewashukuru waajiri wa sekta rasmi, wanachama na wananchi waliojiajiri kwa ushirikiano wao na NSSF, akisema ushirikiano huo ni muhimu katika kuhakikisha huduma za Hifadhi ya Jamii zinawafikia wananchi wengi zaidi.

Pia amewataka waajiri kuhakikisha michango ya wafanyakazi inawasilishwa kwa wakati ili kulinda haki zao.

Amesema NSSF inaendelea kutekeleza mpango wa msamaha wa tozo kwa waajiri watakaolipa madeni yote ya michango ya msingi na kuendelea kuwasilisha michango kwa wakati hadi Desemba 31, 2026, huku akisisitiza kuwa watumishi wa Mfuko wataendelea kuzingatia uadilifu, uwajibikaji, weledi na utu katika utoaji wa huduma.

Akizungumza kuhusu kaulimbiu ya mwaka huu ya “Huduma Bora kwa Vitendo,” Mdabi amesema NSSF itaendelea kuboresha huduma kupitia elimu, ufuatiliaji na maboresho ya mifumo, ili kila mwanachama, mwajiri na mstaafu apate huduma inayostahili kwa wakati na kwa ufanisi.

Wastaafu walioshiriki maadhimisho hayo wamepongeza maboresho yanayoendelea kufanywa na NSSF katika utoaji wa huduma, hususan kupatikana kwa huduma kwa njia ya kidijitali na kupungua kwa muda wa kushughulikia madai ya mafao.

Wamesema maboresho hayo yamerahisisha upatikanaji wa huduma na kuokoa muda, huku wakiiomba NSSF kuendelea kuboresha mifumo yake na kutoa elimu zaidi kwa wanachama na wastaafu kuhusu namna ya kutumia huduma hizo.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi, akizungumza Oktoba 5,2026 wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 yaliyofanyika katika Ofisi za NSSF Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde
Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi, akizungumza Oktoba 5,2026 wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 yaliyofanyika katika Ofisi za NSSF Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi, akizungumza Oktoba 5,2026 wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 yaliyofanyika katika Ofisi za NSSF Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi, akizungumza Oktoba 5,2026 wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 yaliyofanyika katika Ofisi za NSSF Mkoa wa Shinyanga.
Keki maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja NSSF 2026 katika Mkoa wa Shinyanga.
Keki maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja NSSF 2026 katika Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi, akiwa pamoja na wateja wa NSSF wakikata keki maalum katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 yaliyofanyika katika Ofisi za NSSF Mkoa wa Shinyanga.

Post a Comment

0 Comments