
Kambi ya Nyani, kundi la vijana Machachari kutoka Shinyanga, limeendelea kuonesha ubunifu katika tasnia ya muziki baada ya kuachia wimbo mpya unaoitwa “Wanga”, likimshirikisha Dayoo na Michu.
Wimbo huo ambao umetoka ukiwa na video rasmi (Official Music Video), unawakutanisha wasanii hao katika kazi moja ya kimuziki inayolenga kuwafikia mashabiki wa burudani ndani na nje ya Mkoa wa Shinyanga.
Kupitia kazi hiyo, Kambi ya Nyani inaendelea kujitambulisha katika tasnia ya muziki huku ikionesha nafasi ya vijana wa Shinyanga katika kukuza sanaa na burudani nchini.
Ushirikiano na Dayoo pamoja na Michu umeongeza nguvu katika kazi hiyo, ambayo sasa inapatikana kwa mashabiki kupitia mtandao wa YouTube.
Tazama video rasmi ya wimbo Wanga hapa:
0 Comments