Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YARIDHISHWA NA MIRADI SINGIDA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheriaya hiyo Najma Murtaza Giga (katikati) akizungumza na Wanachuo cha Ufundi Veta Mkoa wa Singida na wadau wengine baada ya Wajumbe wa kamati hiyo kutembelea chuo hicho jana. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida, Selemani Mwenda na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira,Vijana na Wenye Ulemavu Profesa Jamal Katundu.




Wajumbe wa kamati hiyo wakipata maelezo walipotembelea karakana ya mitambo mbalimbali chuo cha Veta Singida.
Wajumbe wa kamati hiyo wakinunua bidhaa za wajasiriamali waliowezeshwa na Serikali.
Wajumbe wa kamati hiyo wakipata maelezo walipotembelea banda la Mjasiriamali aliyetengeneza majiko kwa kutumia teknolojia ya udongo na mabati.
Wajumbe wa kamati hiyo wakipata maelezo walipotembelea SabaSaba Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu.
Afisa Vijana Mkoa wa Singida Frederick Ndahani akizungumza na Wanafunzi wa SabaSaba Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu wanaojifunza kushona nguo.
Wanafunzi wa SabaSaba Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu wakiwa kwenye hafla ya kuwapokea wajumbe hao.
Wanafunzi wa SabaSaba Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu wakiwa kwenye hafla ya kuwapokea wajumbe hao.
Mkuu wa chuo hicho, Fatma Malenga akisoma taarifa ya chuo hicho kwa wajumbe wa kamati hiyo.
Wanafunzi wa Chuo cha FDC wakiwa kwenye hafla ya kuwapokea wajumbe hao.
Wajumbe wa kamati hiyo wakitoka kukagua jengo la TEHAMA la Chuo cha FDC.
Wajumbe wa kamati hiyo wakikagua Ofisi ya Udhibiti Ubora wa Shule Manispaa ya Singida.







Na Dotto Mwaibale, Singida



KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imekagua na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya vijana iliyopo mkoani hapa.

Wakati huo huo Wajumbe wa kamati hiyo wamewataka vijana kuchangamkia fursa ya program ya kukuza ujuzi kwa vijana inayofadhiliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwani itawakomboa kiuchumi.

Ombi hilo limetolewa jana kwa nyakati tofauti na wajumbe wa kamati hiyo wakati wa ziara yao ya siku moja ya kukagua miradi ya maendeleo ya vijana iliyopo Manispaa ya Singida.

Wajumbe hao waliwasihi vijana hao kujikita zaidi kwenye mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kujiajiri na kuondokana na dhana ya kutaka kuajiriwa.

Mafunzo wanayojifunza ni ya fani za umeme, ushonaji nguo, mapambo,useremala,ujenzi na kupaka rangi.

Miradi waliyoitembelea ni ile ya vijana waliowezeshwa na Serikali kupitia asilimia nne ya mapato ya ndani.

Awali akitoa neno la utangulizi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira,Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Profesa Jamal Katundu alisema nia ya kamati hiyo kwenda Singida ni kutokana na kazi nzuri ya miradi walioifanya kwa asilimia 100 na kupitishwa bila ya kukataliwa kufuatia usimamizi mzuri wa vikundi vya vijana mkoani hapa.

Katika ziara hiyo wajumbe hao walipata fursa ya kuzungumza na vijana wanaopata mafunzo mbalimbali ya ufundi katika vyuo vya Veta, FDC, na SabaSaba Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu ambapo pia walitembelea miradi yote iliyozinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru na kukagua bidhaa za vijana hao kwenye Maonyesho yaliyofanyika Chuo cha Veta yaliyo andaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo waliokuwa kwenye ziara hiyo ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Watu Wenye Ulemavu, Ummy Nderiananga, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira,Vijana na Wenye Ulemavu Profesa Jamal Katundu na Mwenyekiti wa kamati hiyo Najma Murtaza Giga.

Post a Comment

0 Comments