Ticker

6/recent/ticker-posts

RC MAKALLA KUANZA ZIARA YA KUTATUA CHANGAMOTO ZA MIGOGORO MKOANI DAR ES SALAAM



- Ni sehemu mkakati wake wa kuwafikishia wananchi msaada wa kisheria kwenye maeneo yao.




- Awaalika Wenye Migogoro kuwasilisha kero zao.




- Asema kila mmoja atapata haki yake kwa mujibu wa Sheria.




- Awaandaa wataalamu wa sekta mbalimbali kwaajili ya kuhudumia kila atakaefika.




Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla anatarajiwa kuanza rasmi ziara ya kusikiliza na kutatua kero na changamoto za Wananchi wa Mkoa huo Jimbo kwa Jimbo ikiwa ni Mpango wake wa kupatia ufumbuzi kero za Wananchi.




RC Makalla amesema ziara hiyo itaanza rasmi Jumatatu ya August 30 kwenye Jimbo la Kawe Viwanja vya Tanganyika Packers, August 31 Jimbo la Kibamba, September 01 Jimbo la Segerea, September 02 Jimbo la Mbagala na September 03 Jimbo la Kigamboni ambapo zoezi litaanza kuanzia Saa mbili Asubuhi Hadi majira ya jioni.




Aidha RC Makalla amesema kutakuwa na jopo la Wataalamu wabobezi wakiwemo Watendaji wa Serikali, Wanasheria, Kamishina wa Ardhi, Maafisa Ardhi, Jeshi la Polisi, TAKUKURU na Wadau wote wanaojihusisha na masuala ya kisheria.




Pamoja na hayo RC Makalla ametoa wito kwa Wananchi wote Wenye Migogoro kutumia Fursa hiyo kuwasilisha Malalamiko yao ili yaweze kupatiwa ufumbuzi kwa mujibu wa Sheria.






Post a Comment

0 Comments