Ticker

6/recent/ticker-posts

TBS YATOA WITO KWA TAASISI ZINAZOJIHUSISHA NA UGEZI NA ITHIBATI YA UBORA KWENDA KUPATA MAFUNZO

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa wito kwa Taasisi binafsi na za kiserikali zinazojihusisha na ugezi, ithibati ya ubora kwenda kupata mafunzo ya ithibati ili kuwawezesha kuweka mifumo ya kimataifa katika utendaji wa kazi zao.


 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mratibu anaesimamia dawati la ithibati Bi.Stella Mroso amesema kuwa ithibati inaweza kutolewa kwenye taasisi za upimaji, ukaguzi, uthibiti wa ubora ikiwa na lengo la kujenga imani kwa watumiaji wa bidhaa au huduma kuona inafaa kwa matumizi.


 "Ithibati ni nyenzo muhimu katika kuondoa vikwazo vya kibiashara kitu ambacho kitachangia kukuza uchumi wa Taifa letu hasa katika Uchumi wa viiwanda". Amesema Bi.Stella. 


Aidha Bi.Stella ameelezea manufaa ya kutekeleza mifumo ya kiwango cha kimataifa katika maabara za upimaji za ugezi ambapo moja ya manufaa ni kujenga imani kwa wateja, kuziwezesha maabara kufafanua na kuainisha kazi zao lakini pia kuweka malengo ya ubora katika kufikia malengo ya taasisi.


 Hata hivyo ameelezea ni maandalizi gani kama maabara wanatakiwa kuwa nayo ambapo kabla ya kuomba cheti cha ithibati ya umahili moja ya maandalizi ni kupata uelewa wa matakwa ya viwango husika kwa kupatiwa mafunzo ambayo yanatolewa na TBS, hatua nyingine ni kufuata matakwa ya yaliyowekwa ya kimataifa.

Mratibu anaesimamia dawati la ithibati Bi.Stella Mroso akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TBS leo Jijini Dar es Salaam.

Mratibu anaesimamia dawati la ithibati Bi.Stella Mroso akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TBS leo Jijini Dar es Salaam.Pembeni kwake ni Meneja wa Upimaji (TBS), Bw.Joseph Makene.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments