Mkurugenzi wa Mawasiliano, Bi.Rosalynn Mworia akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni mpya ya KIMBIZA NA 4G YA UKWELI uliofanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kanda ya Dar es salaam na Pwani wa Kampuni ya Vodacom Bi.Brigita stephen akizungumza katika uzinduzi wa kampeni mpya ya KIMBIZA NA 4G YA UKWELI uliofanyika leo Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji wa vipindi vya burudani Wasafi Fm na Wasafi Tv, Bw.omary Tambwe maarufu Lil Ommy akizungumza katika uzinduzi wa kampeni mpya ya KIMBIZA NA 4G YA UKWELI uliofanyika leo Mlimani City Jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
******************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Kampuni ya Mtandao wa Vodacom Tanzania mpaka Sasa umeshapeleka mtandao wa 4G kwenye vituo zaidi ya 1800 na katika mwaka huu wa fedha wamezindua vituo 400 vya 4G Tanzania nzima.
Ameyasema hayo leo Mkurugenzi wa Mawasiliano, Bi.Rosalynn Mworia wakati wa uzinduzi wa Kampeni mpya ya KIMBIZA NA 4G YA UKWELI uliofanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia katika uzinduzi huo Bi.Rosalynn amewataka wale ambao hawajapata fursa hiyo awaweze kutumia mtandao wa Vodacom ili waweze kuunganishwa na ulimwengu wa kidigitali kwa kutumia mtandao wa 4G wenye kasi zaidi na kuweza kufurahia huduma hiyo katika maeneo mengi ambayo mwanzo hayakuweza kufikiwa kwa urahisi.
"Uzinduzi huu unaenda kugusa Maisha yetu tofautitifauti, Kuna wafanyabiashara wadogowadogo, wafanyabiashara wakubwa, wakina Mama lishe wanaweka vitu vyao kwenye mitandoa ya kijamii, hii yote imewezakana kutokana na data". Amesema Bi.Rosalynn.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ufundi wa Mtandao- Vodacom, Bw.Andrew Lupembe amesema wamekuwa na minara zaidi ya 3,300 Tanzania nzima ambayo zamani ilikuwa inatoa huduma za 2G ambapo wakaanza kuweka huduma za 4G ambayo inaleta ukuaji wa teknolojia ya data.
"Hadi sasa tuna zaidi ya minara 1800 ambayo inacover zaidi asilimia 60 ya wananchi kwenye mtandao wa data kwa wote".Amesema bw.Lupembe.
0 Comments