Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA ALFAJIRI YA LEO DODOMA,AZUNGUMZIA UVIKO -19



Na Abubakari Akida, MOHA

Serikali imewataka abiria wanaosafiri mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi kuchukua tahadhari juu ya maambukizi ya UVIKO -19 huku wakiaswa kupaza sauti zao pindi wanapoona uvunjifu wa sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazosababisha vifo na majeruhi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Khamis Hamza Chilo alipofanya ziara, alfajiri ya kuamkia leo, lengo ikiwa kutoa tahadhari kwa wadau wa vyombo vya usafiri juu ya tahadhari ya ajali wawapo barabarani sambamba na kujikinga na maambukizi ya UVIKO-19 kwa abiria hao.

“Sasa kuna janga la UVIKO-19 nawaomba muwe makini mkiwa safarini,vaeni barakoa na tumieni vitakasa mikono lakini pia nawaomba mpaze sauti zenu pindi muonapo uvunjifu wa sheria za usalama barabarani,nchi hii inawategemea sana katika kuleta maendeleo na serikali haipendi kuona watu wake wakipoteza viungo na Maisha,askari wetu wako kila sehemu huko barabarani toeni taarifa” alisema Naibu Waziri Chilo

Akizungumzia madereva wanaoenda mwendokasi bila kufuata sheria za usalama barabarani Naibu Waziri Chilo alisema tayari serikali ishaanza utaratibu wa kuchukua leseni ya udereva kwa dereva yoyote atakaethibitika kusababisha ajali kwa uzembe wake.

“Hivi karibu mmeona jinsi dereva wa basi la Sauli linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Tunduma alivyoyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari sasa ile ni hatari, ametokea Mbeya mbali kweli anakuja kupata ajali Kibaha alikuwa na haraka gani? tayari serikali kupitia mamlaka husika ikiongozwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Wilbrod Mutafungwa tushachukua leseni yake na tumemfungia kwa muda wa miezi sita na sasa atarudi darasani akajifunze upya udereva, kwenye kulinda maisha ya wananchi hatutaki mchezo” alisema Naibu Waziri Chilo

Akizungumza kwa niaba ya madereva wengine, Dereva wa Basi la Al Saedy, Alex Emmanuel aliomba elimu itolewe kwa madereva wa malori kwani ndio wamekua chanzo cha ajali nyingi za barabarani hali inayopelekea kutokukoma kwa matukio ya ajali huku Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Boniface Mbao akiweka wazi kuwepo kwa utaratibu wa wa utolewaji wa elimu na ukaguzi wa mabasi kabla ya kuanza safari na basi linalokutwa na hitilafu basi huzuiwa lisiondoke.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Khamis Hamza Chilo akizungumza na abiria wanaosafiri kwenda mikoa mbalimbali nchini wakati wa ziara aliyoifanya alfajiri ya leo lengo ikiwa kuwakumbusha wasafiri kupaza sauti waonapo viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani huku pia akiwaasa kuchukua tahadhari juu ya maambukizi ya UVIKO-19. Ziara hiyo imefanyika leo,Kituo Kikuu cha Mabasi cha Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Boniface Mbao akizungumza na abiria wanaosafiri kwenda mikoa mbalimbali nchini wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo aliyoifanya alfajiri ya leo lengo ikiwa kuwakumbusha wasafiri kupaza sauti waonapo viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani huku pia akiwaasa kuchukua tahadhari juu ya maambukizi ya UVIKO-19. Ziara hiyo imefanyika leo,Kituo Kikuu cha Mabasi cha Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Khamis Hamza Chilo akitoka ndani ya Basi la Kimbinyiko ambako alikuwa akizungumza na abiria wanaosafiri kwenda mikoa mbalimbali nchini wakati wa ziara aliyoifanya alfajiri ya leo lengo ikiwa kuwakumbusha wasafiri kupaza sauti waonapo viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani huku pia akiwaasa kuchukua tahadhari juu ya maambukizi ya UVIKO-19. Ziara hiyo imefanyika leo,Kituo Kikuu cha Mabasi cha Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Post a Comment

0 Comments