Ticker

6/recent/ticker-posts

BAHATI NASIBU NI NINI? WASHINDI WA TUSUA MAPENE WAELEZEA

Mshindi promosheni ya Vodacom wa zawadi kubwa ya Tusua Mapene Tsh 179,000,000, Ramadhani Ismail Bwaniki akikabidhiwa zawadi yake kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Bi Esther Alexander Mahawe katika hafla iliyofanyika uwanja wa katubuka mkoani Kigoma mwishoni mwa mwezi Juni.


*************************

Mwezi wa saba mwaka huu, shindano la Vodacom Tanzania la “Tusua Mapene” lilitangaza ushindi wake mkubwa katika awamu ya nne ya shoindano la kwanza, ambapo mshindi mkuu akijinyakulia Shilingi milioni 180.

Vodacom Tanzania ilianzisha shindano la Tusua Mapene miaka minne iliyopita kwa lengo la kuwazawadia wateja wake waaminifu na kuwapa nafasi ya kutimiza ndoto zao na kuleta mabadiliko makubwa kwa kutumia viwango vidogo kuanzia Shilingi mia tatu kwa siku hadi Shilingi 6,000 kwa kifurushi cha mwezi chenye unit 30. Katika kipindi hiki, Tusua Mapene imetoa jumla ya Shilingi bilioni 4 kama zawadi kwa washindi zaidi ya milioni 500. Wahindi hawa wa mashindano ya kila siku, ya wiki, ya mwezi na mashindano makuu zenye zawadi kuanzia shilingi 15,000 hadi milioni 20 za kila siku hadi milioni 100 na zaidi katika kumalizia ngwe moja kwenda nyingine.

Tukiangalia washindi waliopita wa shindano hili, tunaona mabadiliko. Celestine Kilemezi wa Musoma, aliyeshinda milioni 128 alitumia ushindi huo kujenga nyumba, kununua gari na kiwanja. Ilikua tukio la kutoaminika aliposhinda. Anakumbuka kupewa taarifa kuwa anaweza kuwa msindi na kutoamini kwanza.

“Nilipigiwa simu mchana huo na kuambiwa kutazama TBC1 jioni kwani naweza kuwa mshindi. Nilidhani ni wale matapeli tu na nikaendelea na shughuli zangu.” Celestine anaeleza. “Nilipata mshangao mkubwa mjukuu wangu aliponiletea simu saa moja usiku na nikaambiwa kwenye kipindi cha televisheni kuwa nimeshinda!”

Celestine anaendelea kueleza kuwa hakukuwa na matatizo yoyote kupokea ushindi wake kwani alipigiwa simu na maafisa wa Vodacom waliopanga naye siku ya kukutana na kumkabidhi hundi yake. Baada ya kupokea pesa zake, alinunua nyumba mjini Mwanza, gari jipya na viwanja vitatu ambavyo anajenga.

Aliyoyaona katika kushiriki kwake, anasema, kumemjengea imani kuwa bahati nasibu inayoendeshwa na Vodacom ni ya haki na haina upendeleo. “Kuna wau wanaamini kuwa michezo hii si haki na washindi wanakuwa wamekwisha pangwa. Niko hapa kuwaambia kuwa hii si kweli. Kwenye mchezo huu wa Vodacom, mimi sikuwa na uhusiano na waandaaji wala sina ndugu wala marafiki katika kampuni. Nawashauri wengine kushiriki, nao pia wanaweza kushinda kama nilivyoshinda mimi,” anaongeza Celestine.

Wakati wa makabidhiano, Mkurugenzi wa Dijitali na huduma za ziada wa Vodacom Tanzania, Bwana Nguvu Kamando alisema, “Lengo la Tusua Mapene ni kuwawezesha Watanzania kiuchumi. Nawahimiza wateja wetu kushiriki katika shindano hili linaloendelea kwa sababu kwa kufanya hivyo unajipatia nafasi ya ushindi mkubwa.”

Mwanzoni mwa mwaka 2020, Eveneth Rutiyomba ambaye ni mkazi wa Dar es Salaam alishinda Shilingi milioni 150. “Hii ni ndoto kwangu,” alisema, “sikutegemea hata siku moja kuwa ningeshika pesa nyingi kiasi hiki maishani mwangu, lakini leo hii niko hapa na maisha yangu yamebadilika kabisa.”

Mshindi mwingine, Marko Kilungala, mwenye umri wa miaka 47, alishinda zaidi ya Shilingi milioni 80 na alitumia pesa hizo kununua kiwanja amabapo amejenga nyumba anayosihi kwa sasa. Alisungua akaunti benki alipoweka pesa zilizobaki na, baada ya muda kutimia, anatueleza kwa kujivunia kuwa alichukuwa pesa hizo na kununua trekta anayotumia kufanyia kilimo na pia kama chanzo cha mapato, huku akituonyesha vifaa na uwezo wa trekta yake mpya.

Lakini hakuishia hapo tu. Kwa kuwa na mikakati ya uwekezaji, ameweza kuongeza pesa alizoanza nazo. Kama Marko mwenyewe anavyosema, “nilihitaji usafiri kwa hiyo nikanunua piki piki. Nika nunua pia pikipiki nyingine nne kama uwekezaji na kuingia nazo mikataba. Nategemea kurudisha pesa nilizonunulia ifikapo mwezi wan ne mwakani na hivyo nitaweza kuwekeza katika maeneo mengine zaidi.”

Maisha ya Marko yamebadilika kabisa na mabadiliko hayo anaeleza yanatokana moja kwa moja na Tusua Mapene.

Kwa muda wa mashindano kumekuwa na washindi wengine wakubwa. Mshindi wa kwanza kabisa wa ngwe ya kwanza akiwa ni Bw. Jaxkson A. Mwankemwa mwenye umri wa miaka 51, mkulima kutoka Kijiji cha Msasani wilayani rungwe mkoani Mbeya aliyejishindia Zaidi ya Shilingi milioni 200.

Mashindano ya Tusua Mapene sasa yameingia awamu nyingine ambapo mshindi mkuu mwingine atapatikana na Maisha yake kubadilika milele. Shindano hili ni njia mojawapo ambayo Vodacom Tanzania Plc inatumia mtandao wake mpana na idadi kubwa ya wateja kunufaisha Watanzania. Lakini pia, rusisahau kuwa kuna washindi wengi zaidi, siyo tu washindi wa zawadi kuu, bali pia zawadi za kila siku, za kila wiki na za kila mwezi, ambazo nazo ni za viwango vyenye thamani kubwa na kuweza kuleta mabadiliko chanya maishani mwa washindi hao kiuchumi.

Ushiriki wa shindano ni rahisi. Mteja anatakiwa kutuma ujumbe wenye neon “Check” kuenda namba 15544 ili kujiunga. Baada ya hapo, ataweza kutumia huduma ya M-Pesa kununua vifurushi vya kila siku, kila wiki au vya mwezi kuendana na matakwa yake mwenyewe.

Post a Comment

0 Comments