Ticker

6/recent/ticker-posts

FIFA YATHIBITISHA JAPAN KUJIONDOA KUANDAA MICHUANO YA KLABU BINGWA YA DUNIA DESEMBA MWAKA HUU






Shirikisho la soka duniani (FIFA) limethibitisha kwamba Japan imejitoa kwenye kuandaa michuano ya Klabu bingwa ya Dunia iliyotakiwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu.

FIFA ilipokea maombi kutoka shirikisho la soka la nchini Japan (JFA) likiomba kutoandaa michuano hiyo kwa hofu ya gonjwa la Uviko-19 hivyo shirikisho la soka, FIFA limeyapokea maombi hayo na kuthibitisha kwamba michuano hiyo haitofanyika tena nchini humo.

Bado haijafahamika mashindano hayo yatafanyika wapi mpaka sasa..

Post a Comment

0 Comments